ALIYEKUWA
mchumba wa msanii wa filamu Bongo, marehemu Sheila Haule ‘Recho’,
George Saguda amesema baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhan, sasa anajiandaa kwa ajili ya kisomo cha kumkumbuka mwenzake
huyo.
Marehemu 'Recho' na aliyekuwa mpenzi wake George Saguda wakiwa ni wenye furaha pamoja enzi za uhai wake.
Akipiga stori na gazeti hili, Saguda alisema zilipotimia siku 40,
kilifanyika kisomo kwa bibi wa marehemu huko Songea, lakini kwa vile
Recho alikuwa akiishi Dar es Salaam na wasanii wenzake wapo huko, yeye
anajipanga kufanya kisomo maalum kwa ajili ya mchumba wake huyo ambaye
hawezi kumsahau milele.
“Baada ya Ramadhani kumalizika nitafanya kisomo kwa ajili yake na
mwanangu ili Mungu awapunguzie adhabu ya kaburi, pia kwa walioenda
kuweka tunguri kwenye kaburi lake, kama walikuwa na nia mbaya Mungu
aepushe maana nikisema niende kwa waganga nitakuwa napoteza muda tu
kikubwa namtegemea Mungu,” alisema Saguda.
0 comments:
Post a Comment