
Basi hicho ndicho kitakachotokea kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini
litakalotimua vumbi Agosti 8, 2014 (Nane Nane) kwenye Uwanja wa Taifa
ambapo waheshimiwa hao watanyukana live ulingoni katika pambano lisilo
la ubingwa kumsaka mshindi.
Achilia mbali wabunge hao, pia mastaa kibao watakung’utana; Jacqueline
Wolper atapanda ulingoni dhidi ya msanii mwenzake wa kike, Cloud 112 wa
Bongo Muvi na Jacob Steven ‘JB’ nao
watavurumishiana makonde bila kumsahau mwanamuziki wa Mapacha Watatu,
Khalid Chokoraa atakayezichapa na Said Memba huku mashabiki
watakaohudhuria pia wakipata burudani ya ndondi kali kutoka kwa Bingwa
wa Afrika Mashariki na Kati, Thomas Mashali dhidi ya Mada Maugo.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, shughuli haitaishia hapo kwani
kutakuwa na burudani ya muziki wa Injili. Watumishi wa Mungu wanaoimba
nyimbo za Injili, Upendo Nkone, Ambwene Mwasongwe, Angela, Paul Clement,
Martha Mwaipaja na wengine wengi watakuwepo uwanjani hapo.
“Pia mkali wa ngoma ya Johnny, Yemi Alade kutoka nchini Nigeria
atakuwepo ndani ya nyumba kuoneshana kazi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’,
achilia mbali Ali Kiba atakayezikonga nyoyo za mashabiki wake waliommisi
kwa kipindi kirefu,” alisema Maloto.
Pia aliongeza kuwa kutakuwa na wasanii wengine kibao wakiwemo Madee,
R.O.M.A Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi
na kwa mara ya kwanza Wema Sepetu atapanda jukwaani na kuimba nyimbo za
bebi wake ‘Diamond.’
Kwa upande wa soka, Maloto alisema kutakuwa na mechi kati ya Wabunge
Mashabiki wa Yanga dhidi ya wenzao wa Simba, timu ya Bongo Muvi
itapepetana na Bongo Fleva sambamba na Azam watakaokipiga dhidi ya
Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Maloto aliongeza kwamba mshindi wa Shindano la Amani Talent Search,
Paschal Dominic ‘P-Plan’ naye ameongezwa kwenye listi ya wasanii
watakaomua kwenye shoo hiyo kubwa na ya kihistoria.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E FM (93.7), Clouds FM (88.5), Syscorp pamoja na Times FM (100.5).
Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E FM (93.7), Clouds FM (88.5), Syscorp pamoja na Times FM (100.5).
0 comments:
Post a Comment