Leo nataka kuzungumzia namna unavyoweza kusherehekea Sikukuu ya Idd wakati mpenzi wako akiwa mbali na wewe.

Najua namna ambavyo sikukuu inaweza kuwa mbaya kwa kiasi f’lani kwa
kumkosa uliyetokea kumpenda lakini kwa kuwa imetokea hivyo, chukulia ni
hali ya kawaida ila kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ili uwe
na furaha siku hiyo.
MawasilianoHakikisha siku hiyo simu yako ina muda wa maongezi wa kutosha
na chaji iko ‘full’. Hii ni kwa sababu mawasiliano ya mara kwa mara
lazima yafanyike. Kwa siku hii haiwezi kuwa kero, mpigie simu kila
unapojisikia na yeye kwa kuonesha kukujali anatakiwa kupokea.
Pia sms nzuri ndiyo wakati wake. Muandikie nyingi kadiri unavyoweza na
yeye pia ili kukufanya ujisikie mwenye amani, atatakiwa kukujibu haraka
iwezekanavyo.
Hii ni mbinu ya kujiweka karibu naye na endapo utaitumia simu yako
ipasavyo, hutajisikia mpweke na siku yako itapita huku ‘ukiwa na mpenzi
wako’.
Zawadi!
Hiki ndiyo kipindi chake. Siku hii muandalie zawadi ambayo itamfanya ajione umemthamini sana. Zipo zawadi zinazoshauriwa kwa kipindi hiki cha sikukuu.
Hiki ndiyo kipindi chake. Siku hii muandalie zawadi ambayo itamfanya ajione umemthamini sana. Zipo zawadi zinazoshauriwa kwa kipindi hiki cha sikukuu.
Kwa mfano, unaweza kumnunulia nguo, viatu, vipodozi na vitu vingine
ambavyo atavitumia siku hiyo. Kwa zawadi hizo ni lazima popote
atakapokuwa atajisikia yuko nawe.
Jua atatoka na nani kwenda wapi
Ni vizuri sana kujua huko aliko atatoka na nani kwenda wapi. Katika mazingira haya siyo mbaya kufanya ushushushu kujua kama atakavyokuambia ni sahihi.
Ni vizuri sana kujua huko aliko atatoka na nani kwenda wapi. Katika mazingira haya siyo mbaya kufanya ushushushu kujua kama atakavyokuambia ni sahihi.
Ni vizuri pia huyo anayetoka naye ukawa na mawasiliano naye na awe ni
mtu unayemuamini. Mfuatilie kwa karibu na wala usimuache akajichunga
mwenyewe. Najua unaweza ukawa unamuamini lakini kujiaminisha zaidi siyo
mbaya.
Nasema hivi kwa kuwa, sote tunajua siku za sikukuu zinavyokuwa. Ni siku
ambazo hata wale ambao hawakuwa na mawazo ya kusaliti wanajikuta
wakifanya hivyo.
Wapo ambao walitoka wakiwa wazima lakini wakashawishika kunywa pombe na
wakafanya ambayo hawakudhamiria. Zungumza naye mara kwa mara na
mkumbushe umuhimu wa yeye kujichunga na kutokusaliti kwa kuwa uko mbali
naye.
Muwekee mipaka
Si vibaya pia ukamuwekea masharti na mipaka kwa siku hiyo. Kwa mfano unaweza kumkataza pia asitoke ikishafika saa moja. Awe nyumbani na wewe uwe nyumbani, muutumie muda huo kuzungumza mambo mengi ambayo yatawaliwaza.

Pia suala la pombe unaweza kumtaka asinywe hata akiwa yuko nyumbani.
Hivi utajisikiaje pale ambapo utampigia simu mpenzi wako na yeye
akakuambia yuko nyumbani, amekunywa pombe na amelewa sana?
Hata kama amelewa akiwa nyumbani lakini haileti picha nzuri. Sote
tunajua madhara ya pombe kwa hiyo ni vizuri tukashauriana kutotumia
kilevi hicho.
Mfanyie ‘sapraizi’
Zaidi ya yote, kuna kitu kinaitwa ‘sapraiz’. Kwa lugha ya kawaida neno hili linamaanisha kumfanyia mtu kitu ambacho hakukitarajia. Katika siku za sikukuu wengi wamekuwa wakiwafanyia wapenzi wao ‘sapraiz’ lakini kwa yule ambaye yuko mbali na mpenzi wake ‘sapraiz’ kubwa unayoweza kumfanyia ni kumtembelea.

Hebu jiulize, wewe uko Mwanza na mchumba au mpenzi wako yupo Dar.
Mmekuwa mkiwasiliana na akakueleza kuwa, kutokana na kubanwa na mambo
hataweza kufika huku na wewe pia ukiwa huwezi kumfuata.
Kutokana na mazingira hayo, mnaendelea kuwasiliana lakini siku moja
kabla ya sikukuu, ukijua kabisa yeye atakuwa nyumbani, unapanda gari na
kwenda Dar kisha ukifika unampigia simu na kumwambia aje akupokee
stendi.
Kwanza hataamini kile unachomwambia lakini akishakuona hiyo furaha yake
haiwezi kuelezeka. Wapo waliofanikiwa kufanya ‘sapraiz’ hizo na wameona
jinsi walivyowafurahisha wapenzi wao.
Naomba kwa kumalizia niseme tu kwamba, hakuna kitu kinachouma kama
kusherehekea sikukuu huku mpenzi wako akiwa mbali na wewe. Utakuwa
ukiumia zaidi pale utakapowaona wenzako wakitoka na wenza wao huku wewe
ukiwa mpweke.
Lakini kwa kuwa hiyo yote ni sehemu ya maisha, huna sababu ya kuumia
sana. Kwa kufanya hayo niliyoyaeleza hapo juu, angalau utapata faraja na
naamini siku itapita na maisha mengine yataendelea kuwepo.
Kikubwa ni kuombeana uzima na kila siku kumuomba Mungu uhusiano wenu uwe
ni wenye kutawaliwa na furaha na amani. Wazungu wanasema; Where there
is true love, distance doesn’t matter, wakimaanisha kwamba penye penzi
la dhati na la kweli, umbali siyo tatizo.
0 comments:
Post a Comment