
KATIKA kujiongezea vyanzo vya mapato, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ameamua kujizatiti zaidi kwenye biashara ambapo sasa amefungua sehemu ya kuoshea magari maarufu kama Car Wash iliyopo Tabata, Dar es Salaam.
“Hakuna cha maana ninachopata kwenye filamu zaidi ya umaarufu tu. Wakati marehemu mume wangu (Sajuki) alipokuwa hai alikuwa anakimbizana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lakini mimi kama mtoto wa kike, nashindwa kufuatilia vizuri.
“Kwa sasa nimeamua kujikita zaidi kwenye biashara, filamu nitafanya lakini mara chache. Hapa nasubiri Ramadhani ianze na ipite, natarajia kufungua na hoteli hapahapa baada ya mfungo,” alisema Wastara.
0 comments:
Post a Comment