
MSANII wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ alijikuta akitaka kuangua kilio baada ya kupewa mkono na Rais Jakaya Kikwete wakati wa mazishi ya nguli wa vichekesho nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’.
Akizungumza na paparazi wetu, Sandra ambaye alikuwa akisukuma watu ili aweze kupewa mkono na rais, baada ya kufanikiwa alisema anajivunia kumshika mkono kwani anaamini kwa kushika huko atapata baraka na mambo yake yatamnyookea zaidi ya ilivyo sasa.
“Jamani unajua kushikwa mkono na mkuu wa nchi ni baraka! Yaani hapa roho yangu imetulia na ninaamini nitapata kitu kikubwa na cha maana,” alisema Sandra.
0 comments:
Post a Comment