Saturday, June 28, 2014


IMESUBIRIWA kwa hamu, hatimaye siku imewadia. Leo ndiyo leo, Bendi ya Skylight na Yamoto zinakutana katika steji moja ya Dar Live kuangusha burudani baab’kubwa.
Skyligth wameahidi kupiga nyimbo zote kali sambamba na kutambulisha video yao mpya inayofahamika kama Pasua Twende.


Meneja wa Skylight, Aneth Kushaba alisema mashabiki wafike kwa wingi kwani mbali na uzinduzi wa video hiyo, watatambulisha staili zao mpya za kucheza kama Kwaito, Sebene, Mduara na kuimba mitindo mbalimbali ikiwemo ya Kikongo, AfroPop, RnB na nyinginezo.
“Mashabiki watainjoi staili zetu kali, watatazama kwa mara kwanza video ya Pasua Kichwa katika skrini kubwa, watazisikia nyimbo zetu kuanzia Nasaka Doo, Mbeleko, Kariakoo, Wivu, Carolina na nyinginezo, itakuwa ni swangwe mwanzo mwisho,” alisema Aneth.
Kwa upande wa Yamoto Band, kiongozi wao Said Fela amesema watatambulisha video ya wimbo wao mpya inayofahamika kama Nitajuta.
“Itakuwa ni swangwe tupu, tutaporomosha nyimbo zetu zote kuanzia Birthday, Yamoto na nyingine kibao hivyo mashabiki wetu tunawaomba wafike kwa wingi,” alisema Fela.
Mbali na bendi hizo mbili kukamua kwa mpigo, atakuwepo mkali anayetamba na wimbo wa Sugua Gaga, Sarah Kaisi ‘Shaa’ huku kiingilio kikiwa ni Sh 7000 tu!
Uzinduzi na shoo hizo kali kutoka kwa Skylight na Yamoto Band umedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe