Saturday, June 7, 2014

Marehemu Albert Mangweha.
BAADA ya kusubiriwa kwa hamu, kesho tarehe 8, Juni ndiyo siku ambayo mastaa kibao watadondoka katika jukwaa la Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar kupiga shoo kali ya kumuenzi legendary wa muziki wa Hip Hop Bongo, Albert Mangweha.
Mratibu wa shoo hiyo, Luqman Maloto amesema listi itakayoshuka jukwaani itaongozwa na TID, Chid Benz, Mchizi Mox, Nako 2 Nako, Geez Mabovu, Dark Master, M2 The P, Josline, Squeezer, Nyandu Toz, Inspekta Haroun, Mez- B, H. Baba na Babuu wa Kitaa.

Inspekta Haroun akikamua.
Wasanii hao kwa nyakati tofauti wameiambia Mikito Nusunusu kuwa hawatabakisha wimbo, wataoneshana uhodari wa kuimba nyimbo zao hususan zile walizoshirikiana na marehemu Ngwea.
Maloto amesema shoo hiyo ambayo awali ilikuwa ifanyike leo na kusogezwa hadi kesho, Jumapili, mbali na shoo kali kutoka kwa mastaa hao wa Bongo Fleva, kutakuwa na mtoko maalum wa mastaa wa Bongo Movies akiwemo Jacqueline Wolper, Wema Sepetu na Miss Rashida Wanjara.
Umati wa mashabiki ukiserebuka ndani ya Dar Live.
“Tutakuwa na red carpet, mashabiki watapata fursa ya kupiga picha pamoja na mastaa mbalimbali, huku pia kukiwa na big screen ambayo itaonesha video alizofanya marehemu,” alisema Maloto na kuongeza:
“Vijana wa Shindano la Amani Talent Search watakuwepo pia kuhakikisha wanapagawisha zaidi kwa shoo kali.”

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe