Baada ya diamond kuachia nyimbo yake ya Mdogomdogo mapema wiki hii, hit
single iliyopokelewa vizuri sana na watanzania wengi, huku kila mmoja
akiwa anasubiria kwa hamu jinsi video ya wimbo huo utakavyokuwa, kwa
mujibu wa Diamond Platnumz mwenyewe anasema, wimbo huo ni kwa ajili ya
wa tzee kwanza, ila homa ya jiji na ya bara zima la africa inakuja
mapema wiki ijayo.

Diamond Platnumz ameanza kuwa na utaratibu mpya unaomfanya atoe nyimbo
mbili kwa pamoja, ya kwanza ikiwa kwa ajili ya watzee, na kama fans wa
nchi nyingine hawataielewa, basi kuna nyingine inayotoka hivi karibuni
kwa ajili ya bara zima, hii ni kutokana na staili tofauti anazotumia
kuwakosha nyoyo mashabiki wake wa kila pande za dunia. Sauti ya Iyanya
ndio itakayosikika kwenye nyimbo yake mpya, Iyanya akiwa ni msanii
anayekubalika huko West Africa zaidi hata ya Davido, hii inatarajiwa
kumuweka Diamond Platnumz kwenye ukurasa mpya wa muziki.
0 comments:
Post a Comment