
Wema na Kajala wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa bifu yao iliyopelekea waanze kuonana kama paka na panya
KINACHOGOMBEWA baina ya waigizaji wawili wa Bongomuvi, Wema
Sepetu na Kajala Masanja, ambao awali walikuwa maswahiba wakubwa
hakijajulikana mpaka sasa.
Kila mmoja anamrushia mpira mwenzake kwamba ndiye
mwenye makosa na mwanzilishi wa sekeseke ambalo limewagawanya mashabiki
pande mbili.
Maneno yameendelea kurushwa na watu wasiofahamika
ikidaiwa kuwa wahusika ni wasanii hao. Hivi karibuni Kajala alisafiri
kwenda China na safari ikazua maneno lukuki kwamba ilikuwa ikimhusisha
pia mpenzi wa zamani wa Wema.
Mpaka sasa mwigizaji huyo inasemekana yupo na mtu
huyo licha ya kwamba hakuna ushahidi kuhusu hilo. Vyombo mbalimbali vya
habari vimeripoti kuwa vinamsubiri mwigizaji huyo Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Nyerere kumhoji kwa kitendo anachodaiwa kumfanyia swahiba wake.
Kwa upande wa Wema, yeye ameendelea kushikilia
msimamo wake kwamba hana ugomvi na Kajala licha ya kuonekana akiposti
picha wakiwa pamoja kama afanyavyo Kajala. Hali hiyo imeufanya ugomvi
wao kuonekana kuwa ni wa chinichini mno.
Wawili hao walianza urafiki wao tangu Wema
alipomlipia mwenzake faini ya Sh13 milioni mahakamani na kumwepusha
kwenda jela baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba.
Kajala alitakiwa kulipa faini hiyo baada ya
kupatikana na hatia ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria.
Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino,
kushtakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.
Chanzo
Taarifa zilianza kwamba wawili hawa wanamgombea
aliyekuwa mpenzi wa Wema wa zamani aliyefahamika kwa jina moja la
Clement, ilisemekana kwamba Kajala anatoka na huyo mtu japo mpaka sasa
hakuna ushahidi wa jambo hilo japo baadhi ya watu wameendelea kusema ni
kweli na wameshawaona wawili hao sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Ugomvi huo ulianza wakati Kajala akitengeza filamu
yake ya pili inayoitwa ‘Pishu’ aliyomshirikisha Mzee Senga chini ya
mtayarishaji Lamata.
Wakati wakimalizia filamu hiyo maeneo ya Block 41
huku Kajala akiwa bibi harusi akimpakia Mzee Vengu kwenye baiskeli,
Kajala alilowa sana jasho na kuamua kupitia Saloon maeneo ya Kinondoni
Makaburini na ndipo alipokutana na Wema.
Chanzo hicho kilieleza kuwa Wema alitaka
kumkumbatia, lakini Kajala alikataa na kumzuia kwa mkono kwa sababu ya
jasho na ndio hapo rafiki yake hiyo hakuonyesha kufurahi kwa kitendo
kile.
0 comments:
Post a Comment