MWANAMKE AMTETEA MUMEWE KWA UBAKAJI
LONDON, Uingereza
MWANAMKE mmoja, Adriana Ford-Thompson ambaye ni mhitimu katika chuo kikuu cha Cambridge amejitokeza nakumtetea mumewe, Mark Thompson kwa kosa la kuwavamia wanawake watatu na kufanya nao mapenzi kinguvu.

Adriana 37,alikutana kwa mara ya kwanza na
Thompson nchini Tanzania mwaka 2006 wakiwa katika utafiti wa misitu
aliwaambiwa majaji kuwa bado anampenda mumewe huyo na kwamba ni mtu
mwema na mkarimu licha ya kupatikana kwa kosa la kuteka, kumbaka
mwanafunzi na kuwashambuliwa wanawake watatu kwa kufanya nao mapenzi
kinguvu.
Adrian ambaye kwa sasa ni mtafiti wa
mazingira na mwalimu katika chuo York alimwambia jaji kuwa mara nyingi
alipokuwa akienda ofisini alikuwa akimuacha mumewe nyumbani na pia
hakujua kama kuna mwanafunzi wa chuoni hapo anapofanyia kazi kama
alifanyiwa kitendo cha ubakaji na mumewe.
Baada ya majaji kumhukumu kifungo cha maisha miaka 11 jela mumewe huyo kwa makosa nane ya ubakaji na utekaji kwa wanawake, mkewe alisikika akisema;
Baada ya majaji kumhukumu kifungo cha maisha miaka 11 jela mumewe huyo kwa makosa nane ya ubakaji na utekaji kwa wanawake, mkewe alisikika akisema;
“Thompson ni mtu mkarimu sana, mwema na
matanashati, nimemfahamu miaka kumi iliyopita ni zaidi ya rafiki yangu
wa karibu, nitakuwa pamoja naye kwa kila kitu japokuwa atakuwa mbali na
mimi lakini naamini aliyotenda ni kwasababu hakupata alichostahili.
Thompson ambaye pia ni mtoto wa mchungaji
alijitetea kwa kusema kuwa hakuwahi kufanya mapenzi na mke wake na ndio
sababu iliyopelekea kubaka wanawake hao.
Thompson alitokea Jamaica kwenda kuishi
nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 16 ambapo alikuwa mwana karate
kabla ya mwaka 2006 kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya
utafiti wa misitu.
Alikutana na Adriana nchini Tanzania na mwaka 2007 walirudi Uingereza ambapo walifunga ndoa mwaka 2009.
Alikutana na Adriana nchini Tanzania na mwaka 2007 walirudi Uingereza ambapo walifunga ndoa mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment