Sunday, May 18, 2014

Stori: Adamu Mwanakatwe
MASHOKOLO mageni! Kaka mkubwa kunako kiwanda cha filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukutana na msosi wenye asili ya kigeni na kushindwa ‘kuusosomola’.

Kaka mkubwa kunako kiwanda cha filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray
Tukio hilo lililopigwa chabo na mwanahabari wetu na kuibua hamasa kwa mashuhuda lilitokea juzikati katika Hoteli ya Princes Casino iliyopo Posta jijini Dar, wakati nguli huyo wa filamu alipokuwa katika ghafla ya maandalizi ya safari yao ya kwenda Uturuki kikazi.
Wakati mastaa waalikwa wakienda kuchukua msosi, Ray alichukua sahani lakini alipokuta menu haielewi, alirudisha sahani na kwenda zake kukaa.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe