Wednesday, May 21, 2014


Hosni El Sayed Mubarak.
Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri, Muhammad Hosni El Sayed Mubarak amehukumiwa jela miaka mitatu huku wanae wawili Alaa na Gamal wakifungwa miaka minne kila mmoja.
Waendesha mashitaka wamesema kuwa Alaa na Gamal waliponda mamilioni ya dola ambazo ni pesa za umma zilizotengwa kukarabati ikulu ya Rais na badala yake wakafanyia ukarabati nyumba zao za kifahari.
Watuhumiwa hao wametakiwa kulipa pesa hizo za serikali na kutozwa faini ya dola milioni tatu.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe