Saturday, May 17, 2014


Carles Puyol 

PENZI la lina nguvu sana usisikie. Kwa binti wa Kialgeria, mrembo Wahiba, Franck Ribery hakuwa na ujanja na hatimaye alikubali kubadili dini na kuwa Mwislamu.
Mrembo huyo ndiye alichochea Ribery kubadili dini na jina lake la Kiislamu anaitwa Bilal Yusuf Mohammad.
Hayo ni maisha yake. Kwenye soka, mahali ambapo wengi wanamfahamu Ribery, staa huyo ni hatari. Mkongwe wa soka nchini Ufaransa ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Real Madrid, Zinedine Zidane, aliwahi kumtaja Ribery kuwa ni dhahabu ya soka la Ufaransa.
Soka ndicho kitu kilichomfanya Ribery kuwa maarufu na umahiri wake wa uwanjani umemfanya kuwa mmoja ya wanasoka wanaolipwa vizuri duniani.
Winga huyo wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, aliyezaliwa Aprili 7, 1983, anatajwa kuwa na kipato kinachokadiriwa kuwa Dola 40 milioni.
Jinsi alivyopiga pesa
Chanzo kikubwa cha kipato cha Ribery kinatokana na soka. Ribery anavuna mshahara wa nguvu klabuni Bayern Munich. Mwaka jana, staa huyo aliripotiwa kupanda mshahara kwa Euro 7 milioni kwa mwaka kutoka Euro 3.75 milioni.
Hilo lilikuwa ongezeko kubwa la mshahara ambapo kabla ya kodi alidaiwa kupokea Euro 10 milioni. Taarifa nyingine zilibainisha kuwa mshahara wa Ribery ulikuwa Pauni 8.5 milioni kwa mwaka sawa na Pauni 164,000 kwa wiki.
Hata hivyo, vyovyote itakavyokuwa bado kiwango hicho cha pesa anazopokea staa huyo ni kikubwa.
Ukiweka kando kupiga pesa kwa kupitia mishahara, Ribery pia amekuwa na dili nyingine za mikataba ya udhamini ambayo imekuwa ikimpa manufaa makubwa pia. Baadhi ya kampuni zinazomdhamini staa huyo ni Nike na EA Sports.
Ribery pia anapiga pesa kupitia kipindi chake cha televisheni nchini Ufaransa kinachofahamika kwa jina la ‘The Franck Ribery Show’ ambacho kimekuwa kikivutia wadhamini wengi.
Kipindi hicho cha televisheni kinaonyeshwa kupitia kituo cha Direct 8 na kilikuwa kikidhaminiwa na Nike.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe