Wednesday, May 28, 2014


BIBI kizee aliyetajwa kwa jina moja la Frida amezua kizaazaa cha aina yake baada ya kudaiwa kutokea kimiujiza katikati ya vibanda vya wanawake wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili almaarufu machangudoa hivyo kunusurika kipigo kwa kuhusishwa na mambo ya kilozi au uchawi.


Bibi kizee aliyetajwa kwa jina moja la Frida akisaidiwa chakula na wananchi
Kwa mujibu wa ‘balozi’ wetu, tukio hilo lilijiri Uwanja wa Fisi, Manzese jijini Dar juzikati ambapo awali wakazi wa eneo hilo walidai kumuona bibi huyo tangu alfajiri ya siku hiyo akizungumza mambo yasiyoeleweka ndipo wakamtilia shaka.
Ilisemekana kuwa awali walidhani ni changudoa lakini kadiri muda ulivyosonga ndipo watu wakazidi kumtilia shaka.
Ilidaiwa kuwa ghafla uvumi wa watu kumdhania kuwa ni kigagula (mchawi) ulienea kila kona kiasi cha umati kumzingira huku vibaka wakimkomba hela zote.

Akihojiwa na wananchi baada ya kupewa chakula
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifika eneo la tukio na kuzungumza na bibi kizee huyo ambaye awali alidai alitokea Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Hata hivyo, baadaye alibadilika na kudai kuwa alitokea Keko, Dar na hapohapo Uwanja wa Fisi huku akichanganya madawa kwa kusema ana umri wa miaka 32, jambo lililowashangaza wengi kwani kwa mtazamo wa harakaharaka bibi huyo alikadiriwa kuwa na umri usiopungua miaka 70.
“Mimi nimefedheheshwa sana, nimeitwa malaya, nimefanywa kama mbwa. Mimi nilikuwa na mume wangu James, tulitoka wote Keko-Mwanga (Dar).
“Nina watoto kumi na mbili, tulifika hapa tukienda kwenye nyumba yetu lakini kuna mtu ameiuza na mimi nimefukuzwa ndiyo maana nipo hapa,” alisema bibi huyo aliyeshindwa kuweka wazi mawasiliano ya ndugu zake wa karibu.
Waandishi wetu walifika kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Pakacha, Manzese jijini Dar ambapo walikutana na mtendaji, Ally Mdee ambaye alifika na kumchukua bibi huyo akampeleka kituo kidogo cha polisi cha Tandale huku akitoa rai kwa mtu yoyote anayemfahamu bibi huyo atoe taarifa kupitia simu namba 0652098494.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe