Ukawa kusimamisha mgombea urais 2015
Viongozi wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKawa). Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu. Viongozi hao wapo katika mkakati wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Picha ya Maktaba
Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeanza maandalizi ya kushirikiana katika
Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya
urais, gazeti hili limebaini.
Kadhalika, vyama hivyo ambavyo ni Chadema, NCCR
Mageuzi na CUF vinakusudia kuwa na mgombea mmoja wa nafasi za wabunge na
madiwani, ikiwa ni hatua ya kuzikabili nguvu za chama tawala, CCM.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema tayari
viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekubaliana kuanza mchakato huo na
wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao
kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.
Chanzo chetu kilidokeza kuwa kamati ya wataalamu
kutoka vyama hivyo tayari imeundwa ili kuandaa taratibu zitakazotumika
katika kufanikisha mkakati huo.
Wenyeviti wa vyama hivyo walipoulizwa kwa nyakati
tofauti kuhusu mpango huo hawakukubali moja kwa moja, badala yake
walisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.
Ukawa ni umoja ambao uliviunganisha vyama vyenye
malengo yanayofanana katika Bunge Maalumu la Katiba na vimekuwa
vikishinikiza kuzingatiwa kwa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba hususan muundo wa Muungano wenye serikali tatu, tofauti na
serikali mbili za sasa.
Umoja huo pia uliwaongoza wajumbe wa Bunge Maalumu
ambao ni wanachama wake kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya
kutokana na kile walichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo
yanavyokwenda.
Taarifa za kuwapo kwa mpango wa kushirikiana
katika Uchaguzi Mkuu ujao, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa
mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri kivuli ambalo
litawajumuisha wabunge wa vyama hivyo katika Bunge la Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania.
Baraza la kivuli la sasa linawajumuisha wabunge
kutoka Chadema pekee, ambacho kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni
tangu kuanza kwa Bunge la 10, Novemba 2010.
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema atapanga upya baraza
lake katika siku za mwanzo za Bunge la Bajeti, linalotarajiwa kuanza Mei
6, mwaka huu mpango ambao umeungwa mkono na wenyeviti wa CUF na NCCR
Mageuzi.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema
uamuzi huo ni hatua kubwa katika ushirikiano na kwamba tayari
alikwishawaarifu wabunge wa chama chake wawe tayari kushiriki katika
baraza hilo.
Wenyeviti wa vyama
0 comments:
Post a Comment