Rose Ndauka: Jamani zaeni
ROSE Ndauka ambaye ni mama anayetamba kwenye
filamu za Bongo, amewaonya wasanii wa kike kuachana na biashara ya
utoaji mimba kwani ni kinyume cha maadili na kujidhalilisha.
Alisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu nyota
hawataki kuzaa hata wale waliozaa kabla ya kuwa nyota hawapendi
kujulikana kama wamezaa, kitu ambacho hakina maana katika maisha ya
msanii bali ni kujichelewesha tu.
“Mimi sijui ni kwa nini baadhi ya mastaa hawataki
kuzaa, ni suala la kujipanga tu, kama una kipaji kipo tu hakiwezi
kupotea sababu eti ya kuzaa,” alisema Rose na kuongeza kuwa kadri umri
unavyokwenda na fursa ya kuzaa inapotea na wengi hawajui umuhimu wa
kuzaa mapema.
Ingawa anasema kuna woga wa majukumu ya kulea kwa
baadhi ya vijana wa kisasa na si wasanii peke yao. Rose hivi karibuni
alijifungua mtoto wa kike na kumpa jina la Naveen
0 comments:
Post a Comment