Rooney akiri kuumizwa na Liverpool msimu huu
STRAIKA, Wayne Rooney wa Manchester United amesema inamuuma sana
na kwamba yupo kwenye wakati mgumu wa kuvumilia mafanikio ya mahasimu
wao Liverpool kwenye Ligi Kuu England msimu huu.
Liverpool imekuwa kwenye ubora mkubwa msimu huu na
kupata nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo tofauti na Man United
ambayo ipo kwenye nafasi ya sita.
Klabu ya Liverpool ipo kwenye nafasi ya pili
katika msimamo wa ligi, pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, lakini wao
wakuwa na mchezo mmoja mkononi.
Lakini, kwa upande wa Man United hadithi imekuwa
tofauti baada ya timu hiyo kuwa nyuma kwa pointi tisa kwenye kuifikia
nne bora na hivyo kuzidi kujiweka kwenye wakati mgumu wa kushiriki Ligi
ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
“Kuwatazama Manchester City wakifanya vizuri, sambamba na Liverpool ni kitu kinachoumiza sana,” alisema Rooney.
“Si kitu kizuri hasa ukijifahamu kwamba unaweza
kufanya kitu fulani kwenye ushindani na kisha unashindwa kufanya hivyo.
Tunalifahamu hilo na ndio maana dhamira yetu ya msimu huu ni kuhakikisha
tunamaliza ligi kwa nguvu sana.”
Man United itamenyana na Liverpool kwenye Ligi Kuu England uwanjani Old Trafford, Jumapili hii
0 comments:
Post a Comment