Aliyeiua Man Utd sasa bondia hatari
LONDON, ENGLAND
MAISHA yanaenda kasi na yanabadilika kwa haraka
zaidi. Leon McKenzie, staa wa Norwich City aliyemliza Sir Alex Ferguson
katika pambano la Ligi Kuu England mwaka 2005 sasa ni mmoja kati ya
mabondia hodari Uingereza.
Jumamosi iliyopita, McKenzie alimtwanga bondia
Nikola Varbanov katika raundi ya pili kwenye Ukumbi wa York Hall na
kuendeleza rekodi yake ya kutopigwa pambano lolote katika mechi nne
alizocheza katika ngumi za kulipwa.
Katika pambano hilo ambalo Man United ilikufa 2-0
katika Uwanja wa Carrow Road, McKenzie alikiliza kikosi cha Sir Alex
Ferguson kwa bao murua la pili huku mastaa wa Man United, Cristiano
Ronaldo na Wayne Rooney wakishangaa.
“Alikuwa Rooney ndiye aliyepoteza mpira, Youssef
Safri aliuiba kutoka kwake na kuupeleka pembeni kwa Darren Huckerby
aliyepenyeza mpira kwa Deano na nikamalizia kwa umaridadi,” anasema
McKenzie.
“Nakumbuka wakati timu zikiingia nilimpiga jicho
kali Rio Ferdinand halafu nikajisemea: “leo nitakuonyesha.” Katika soka
unahitaji kwenda uwanjani na kushindana nao. Kuna watu wengine
wananywea, lakini mimi nimetoka katika familia ya ngumi kwa hiyo najua
kupandisha kiwango katika wakati mwafaka.”
Aingia katika soka baba akiwa bondia
Leon ni mtoto wa bondia bingwa wa zamani wa
England na Ulaya, Clinton McKenzie pia baba yake mdogo, Duke McKenzie
akiwa bingwa mara tatu wa zamani wa ubingwa wa dunia.
Leon alianza kucheza soka katika klabu yao ya
mtaani Crystal Palace na mwishowe kusajiliwa katika timu ya wakubwa
kuanzia mwaka 1995 hadi 1996. Mwaka 1997 alitolewa kwa mkopo kwenda
Fulham na mwaka 1998 akaenda zake Peterborough United, ambako alifunga
mabao tisa katika mechi 15.
Mwaka 2003 alihamia Norwich City ambako
alitengeneza jina kubwa kiasi cha kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa
tatu wa klabu katika msimu wa 2004–05, akiwa nyuma ya Darren Huckerby na
Damien Francis.
Msimu wa 2005–06 Leon alijikuta katika wakati
mgumu kutokana na kukabiliwa na majeruhi huku pia akikumbana na wakati
mgumu katika maisha yake binafsi huku akiachana na mkewe.
Mwanzoni mwa msimu wa 2006–07, Leon alimkabidhi
barua ya kuomba kuuzwa kocha wa wakati huo wa Norwich, Nigel Worthington
lakini kocha huyo alikataa maombi hayo huku akidai kwamba klabu hiyo
ingemuuza McKenzie kwa timu ambayo ingetoa ofa nono
0 comments:
Post a Comment