Niyonzima abakizwa Yanga kwa masharti
kiungo wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima
YANGA inapiga hesabu ni nyota gani wanaotakiwa kuachwa katika
msimu ujao, lakini jina la kiungo Haruna Niyonzima limepona baada ya
kuingia makubaliano maalumu na benchi la ufundi.
Taarifa kutoka ndani ya benchi hilo na kamati ya
usajili, imesema katika ripoti iliyowasilishwa na kocha, Hans PLuijm,
imeonyesha kwamba Niyonzima bado anahitajika katika kikosi hicho, lakini
akapewa kazi moja ya kuhakikisha analifanyia kazi tatizo la kutokaa na
mpira muda mrefu kitu ambacho makocha hao hawakitaki.
Bosi mmoja mzito kwenye kamati ya usajili, alisema
Niyonzima ambaye bado ana mkataba wa msimu mmoja na Yanga, ameonyesha
kukubalika na benchi lao la ufundi ambapo sasa anatakiwa kuhakikisha
anakubaliana na mabadiliko hayo aliyotakiwa kuyafanya.
"Ripoti inaonyesha kwamba Niyonzima bado yupo
katika mipango ya kocha na hata mimi nilizungumza na kocha mkuu (Pluijm)
alisema hawezi kumuacha mchezaji kama huyo kirahisi, isipokuwa
ametakiwa kubadilika katika kukaa sana na mpira ni kitu ambacho makocha
hawakitaki," alisema bosi huyo.
Mwanaspoti lilimtafuta Niyonzima ambaye alikiri kuzungumza na Pluijm ambaye amemtaka kulifanyia kazi hilo.
"Nasikia tu katika vyombo vya habari taarifa zangu
kuwa naachwa, najikuta nashangaa. Ni kweli kuwa kocha amenitaka
kubadilika hakuna njia ya mkato kwamba inabidi nilifanyie kazi, ni mambo
mengi tu nimezungumza naye," alisema
RSS Feed
Twitter
10:38 PM
Unknown
0 comments:
Post a Comment