Kaseja ageukia ukocha U-20
YANGA inashuka dimbani leo Jumamosi kucheza dhidi ya watani wao
wa jadi, Simba katika mchezo wa kufunga msimu wa Ligi Kuu Bara lakini
katika kikosi chao hatakuwepo Golikipa, Juma Kaseja ambaye imefahamika
kwamba amepata kibarua cha muda kukinoa kikosi cha vijana chini ya
umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’.
Akizungumza na Mwanaspoti Kocha Mkuu wa Yanga,
Hans Pluijm amsema kuwa walipokea maombi kutoka Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kupitia benchi la ufundi la timu hiyo ya vijana wakiomba
Kaseja aende kuwanoa makipa wao.
Pluijm alisema mara baada ya kupokea barua hiyo
benchi lake lilimruhusu kipa huyo kwenda kufanya majukumu hayo kutokana
na kutokuwepo kwenye kikosi cha wachezaji waanaotarajiwa kushuka
uwanjani kuumana na Simba leo.
“Ni kweli Kaseja hayupo, tulipata taarifa rasmi
kuwa Ngorongoro Heroes ina tatizo la kocha wa makipa, wakatuomba
tuwapatie Kaseja ili akawafundishe makipa wa timu hiyo kwa muda,”
alisema Pluijm.
“Hatukuwa na sababu ya kumzuia kwa kuwa hakuwa
kambini tangu timu ilipokuwa Arusha, tuliona tumpe baraka za kwenda
kuwafundisha vijana hao lakini siyo kwamba hakuwa anahitajika katika
timu.
0 comments:
Post a Comment