Monday, April 21, 2014

Hongereni Azam FC, lakini mbele kuna kazi

 

brahim Bakari 

0
Sha
Naingia tena kwenye ulingo huu wa hoja kuzungumzia mambo yetu yanayotuhusu ya michezo.
Ni wiki ya mafuriko Jangwani na kwingineko baada ya mvua za Masika ambazo mwaka huu haijapata kutokea kufanya ilivyofanya.
Nawatumia tu salamu jamaa zangu kwa mara nyingine, wale walionibishia kuwa Yanga Complex inawezekana Jangwani na walisema niwaachie Yanga yao.
Wapo waliodiriki kuniambia wahandisi ndiyo wenye kufahamu, mimi sijui kitu, sasa sijui leo wataniambia nini na mafuriko hayo.
Haya, tuwaachie hao wanaosema Yanga yao.
Leo nataka kuwapongeza Azam FC kwa kile walichokifanya, kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara baada ya miaka minne ya kuliwinda.
Mara ya kwanza, walimaliza nafasi ya nne, mwaka uliofuata walikuwa watatu, wakashika nafasi ya pili na leo hii ni nafasi ya kwanza, kwa kweli hongereni sana.
Azam FC wanastahili pongezi kwa kuwa waliingia kwenye Ligi Kuu wakiwa na malengo ya kweli katika kuendeleza soka Tanzania.
Wanajipanga kuanzia nyenzo za uwanjani, wamejipanga hata katika rasilimali ya wachezaji kwa kuwekeza katika soka la vijana.
Azam walionyesha kweli wana nia ya ushindi tangu kuanza kwa ligi na ndiyo maana leo hii wamemaliza ligi bila hata kupoteza mechi.
Lakini kikubwa ninachotaka kuwaambia viongozi na benchi la ufundi, ni kwamba wakati umefika wa kutengeneza timu madhubuti kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Ninachokiona kwa upande wangu japo ni utashi wa kocha, kuwa ni wakati wa kusajili wachezaji wenye sifa za kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao walio na tija.
Kama alivyosema awali kocha wa timu hiyo kuwa wachezaji wengi waliopo hawana uwezo wa mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo kuna kila sababu ya kupata wachezaji wenye uwezo.

 

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe