Waziri Christopher ChizaSerikali imetenga hekta 9,000 kwa ajili ya kilimo cha mpunga Wilaya ya
Rufiji mkoani Pwani katika utekelezaji wa mpango wa Uwekezaji mkubwa wa
kilimo katika mikoa ya Kusini (Sagcot).
Akizungumza na wakazi wa kata ya Kipugila, Mkurugenzi wa Saggot, Godfrey
Kirenga, alisema mradi huo upo katika eneo la Rukililo na utakuwa na
uwezo wa kuzalisha tani 250,000 za mpunga kwa mwaka.
Kirenga alisema eneo lilotengwa kwa ajili ya kilimo hicho inajumuisha vijiji vya Ndundunyikanza, Nyaminywili, Kipo na Kipugila.
Alisema idadi hiyo imegawanywa katika sehemu kuu mbili, ambapo hekta
5,000 atapewa mwekezaji mkubwa na hekta 4,000 watamilikishwa wananchi wa
vijiji hivyo.
Kirenga alisema kwa sasa Tanzania inazalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka,
hivyo kiwango hicho kitaifanya nchi kuwa kituo kikuu cha chakula katika
Ukanda wa Afrika Mashariki.
"Nia ya serikali ni kutajirisha wananchi kwa kupitia kilimo katika
mpango huu wa Sagcot mkulima atakuwa na uhakika wa kupata soko pamoja na
uwezeshaji wa kilimo shadidi cha mpunga," alisema.
Aliwataka wananchi wa maeneo hayo kushiriki kikamilifu na kuendelea
kuunga mkono mpango huo wenye lengo la kuwakomboa dhidi ya umaskini.
Alisema kilimo kama hicho kimefanyika Wilaya za Kilombero na Bagamoyo,
ambapo kipato cha mkulima kimepanda kutoka tani sita hadi 11 kwa ekari
moja.
"Nataka niwaambie jambo moja wenzenu kati ya maeneo niliyotaja wameanza
kunufaika kwa sababu hawana tena tatizo la soko kwa sababu wawekezaji
wakubwa wananunua mazao yao kwa bei nzuri," alisisitiza.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Uendelezaji wa Bonde
la Rufiji (Rubada), Aloyce Masanja, alisema mradi huo ambao unasimamiwa
na mamlaka yake, upo katika hatua nzuri na wakati wowote utaanza
utekelezaji wake. Alisema eneo hilo lina ukubwa wa hekta 44,000 lakini
serikali imeamua kulitumia kwa kufuata vigezo vinavyokubalika vya
utunzaji wa mazingira.
"Kabla hatujaanza, mkulima wa kawaida alipata kiasi cha debe tano kwa
ekari moja, nia yetu watoke hapo na kufikia tani sita kwa mwaka,"
alisema Masanja.
Diwani wa kata hiyo, Kassim Mnongane, aliishukuru serikali kwa
kuwapelekea mradi wa aina hiyo ambao utasaidia ukuaji wa kasi wa
maendeleo katika vijiji husika.
Alisema mpaka sasa wamekuwa wakishirikishwa kwa kiasi cha kutosha kwa kila hatua.
Mnongane alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni upotoshwaji
unaofanywa na taasisi zisizo za serikali kwa kuwashawishi wananchi
kutoukubali mradi
0 comments:
Post a Comment