Monday, April 28, 2014

Dk. Mwaka: Matatizo ya mfumo wa uzazi huyumbisha ndoa nyingi

Kuongezeka kwa matatizo ya uzazi kwa familia, ni moja ya sababu zilizochangiwa kuyumba kwa ndoa nyingi ama kupotea kwa matumaini ya kupata watoto.

Akizungumza na NIPASHE Jumamosi,  Dk. Juma Mwaka ambaye ni mtaalam na mkurugenzi wa afya katika kliniki ya  Foreplan  Bungoni jijini Dar es Salaam, alisema baadhi ya matatizo hayo yamechangiwa na ukosefu wa vifaa vya uzazi katika hospitali mbalimbali nchini.

Dk. Mwaka alisema kijiografia matatizo hayo yamesababisha Watanzania wengi wenye matatizo ya kutopata watoto katika ndoa kutafuta njia mbadala.

Kwa mujibu wa Dk. Mwaka, alisema kliniki yake ina takwimu za 2012 ambazo wagonjwa waliofika kupatiwa matibabu wakikabiliwa na matatizo ya uzazi  ni 158,954, wengi wao wakiwa wanawake huku wanaume wakiwa wachache kutokana na waoga.

“Hospitali nyingi hazina vifaa vya uchunguzi wa kina wa mfumo wa uzazi, kutokana na adha hiyo zimeamini baadhi ya vipimo  vya kisasa kama kipimo cha X Ray, Utrasound  ambavyo bado vinaonekana wazi havina uweo wa kubaini ukubwa wa tatizo,”s alisema Dk. Mwaka.

Alisema katika kupanua wigo wa tiba kwa  Watanzania kwa mwaka 2012 hadi sasa ameshafanya ziara katika mkoa wa  Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma pamoja na Iringa.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe