
London, England. Kocha wa Arsenal, Arsene
Wenger amesema anavutiwa na winga wa Leicester, Riyad Mahrez lakini bado
hajatuma maombi ya kumsajili nyota huyo.
Mahrez (26)
amesaini mkataba wa miaka minne na Leicester mwezi Agosti, lakini tangu
wakati huo amekuwa akiomba kuondoka klabu hapo.
Winga huyo alisaidia Leicester kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015-16, kabla ya kumaliza nafasi ya 12 msimu huu.
"Je, tumetuma maombi kwake? Hapana. Hiyo siyo maana kwamba, hilo halitawezekana," alisema Wenger.
Mahrez
alijiunga Leicester akitokea klabu ya Ufaransa ya Le Havre kwa gharama
ya pauni 400,000 mwaka 2014 na 2016 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa
mwaka wa PFA.
"Nafiriki alikuwa na mchango mkubwa kwa
Leicester wakati walipotwaa wa Ligi Kuu, kama ilivyokuwa wengine,"
Wenger aliimbia Bein Sports.
0 comments:
Post a Comment