
KOCHA msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi, amehofia timu
yake kutofanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacom, kutokana na wachezaji
wake wengi waliopo timu za taifa kukosa nafasi ya ku...
Mwambusi ameiambia Goal, anashangazwa kuona asilimia kubwa ya wachezaji wake ndiyo wanaopangwa kwenye timu za taifa za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes zinazoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji nchini Ethiopia kitu ambacho kinawachosha.
“Ni jambo zuri kuitumikia timu ya taifa lakini ikumbukwe mchezaji ni mali ya klabu na sisi kama klabu tunamipango yetu kwa kutegemea nguvu za wachezaji hao ambao hawajapumziko toka mchezo wa mwisho na Kagera Sugar hadi leo,”amesema Mwambusi.
Mwambusi amesema alitarajia katika kikosi cha Kilimanjaro Stars na kile cha Zanzibar Heroes, makocha wangetoa fursa kwa wachezaji wengine badala ya wale wale wa Yanga kila siku, lakini imekuwa tofauti na wachezaji wa Yanga ndiyo wameongoza kwa kutumika wakati wanakabiliwa na ushindani mkubwa kwenye ligi ya Vodacom.
Wachezaji wa Yanga waliopo kwenye michuano ya Chalenji ni pamoja na kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, Kelvin Yondani, Deusi Kaseke, Simon Msuva, Salum Telela na Malimi Busungu na kikosi cha Zanzibar Heroes yupo nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Hajji Mwinyi na Matheo Simon namwengine ni Haruna Niyonzima aliyepo kwenye kikosi cha timu ya taifa lake la Rwanda.
0 comments:
Post a Comment