Thursday, August 27, 2015

Simba yaachana na Papa Niang, zisome sababu hapa
Niang alikuja Simba baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga

SIMBA SC imeachana na Msenegali, Papa Niang baada ya kumjaribu kwa dakika 45 tu jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hawajachoka, Simba SC leo wanatarajia kupokea wachezaji wawili wengine wa kigeni kuwafanyia majaribio, ambao ni Msenegali Pape Abdoulaye N'Daw na Mmali.
N'Daw mwenye umri wa miaka 21, kwa sasa anachezea klabu ya Liga I ya Romania, Dinamo București, wakati wa Mali bado jina lake halijapatikana na haijulikani anatoka timu gani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal kwamba wachezaji hao watafanyiwa majaribio na atakayevutia zaidi, ndiye atapewa Mkataba.
Niang alikuja Simba baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga juu ya dau la usajili.
Niang kutoka klabu ya Alianza F.C. ya El Salvador ambaye ni mdogo wa mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Senegal, Mamadou Niang jana alishindwa kabisa kuwashawishi wana Simba kwa soka yake.
Alichosema Kocha Dylan Kerr
KOCHA wa Simba Dylan Kerr, amesema hakuridhishwa na kiwango cha mshambuliaji mpya rai wa Senegal Papa Niang,aliyepo nchini ka ajili ya majaribio na kusajiliwa na timu hiyo endapo atamridhisha kiwango chake.
Kerr ameiambia Goal nikweli anatafuta mshambuliaji atakaye saidiana na wachezaji waliopo kwenye nafasi hiyo lakini amefadhaishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mchezaji huyo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mwadui FC iliyochezwa Jumatatu uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
“Nikweli nahitaji mshambuliaji lakini siyo wa kiwango kile ndiyo sababu nikampa dakika 45 tu nikamtoa kwasababu hakufanya kile ninachokitaka kwa muda aliocheza aliweza kupiga shuti moja ambao lilipaa juu ya lango baada ya hapo alikuwa mzururaji ndani ya uwanja na kumuona Mussa Hassan ‘Mgosi’ na viungo wakifanya kazi yao vizuri,”amesema Kerr.
Goal ilizungumza na Niang kuhusu kiwango alichokionyesha na mchezo ulivyokuwa na kukiri kucheza chini ya kiwangu huku akisema sababu ni kuwa mapumziko kwa muda mrefu hivyo anahitaji muda wakufanya mazoezi zaidi.
“Ni kweli sijaonesha kiwango kizuri kwasababu nimetoka likizo, na kila sehemu unapokwenda unahitaji muda ili kuzoea, mimi najaribu kuzoea mpira wa Simba. Sifahamiani na wachezaji, nimefanyanao mazoezi kwa siku mbili kwahiyo nilikuwa najaribu kuendana na mfumo wao”, amesema Niang.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe