Friday, August 14, 2015

Preview Manchester City vs Chelsea, hapatoshi ligi kuu wikendi hii
Baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya West Brom ugenini Jumatatu iliyopita vijana wa kocha Manuel Pellegrini watakuwa wakicheza nyumbani mbele ya mashabiki wao

Miamba ya soka nchini Uingereza Manchester City na Chelsea zinatarajiwa kukutana Jumapili hii kwanye uwanja wa Etihad huo ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili kwa timu zote mbili baada ya mechi za ufunguzi zilizopigwa wikend iliyopita.
Baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya West Brom ugenini Jumatatu iliyopita vijana wa kocha Manuel Pellegrini watakuwa wakicheza nyumbani mbele ya mashabiki wao wakimkaribisha kocha Jose Mourinho ambaye katika mchezo wa ufunguzi alilazimishwa sare ya 2-2 na Swansea City akiwa nyumbani kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kwa pande zote mbili kwani kocha wa wenyeji Manuel Pellegrini’s atataka kuendeleza wimbi la ushindi ili kujiendelea kuongoza ligi wakati Jose Mourinho naye atakuwa akitaka kuepuka jinamizi la sare ya nyumbani kwa kupata ushindi mbele ya City iliyomaliza nafasi ya pili msimu uliopita.
Rekodi zinaonyesha Manchester City imeshinda mechi mbili pekee katika mechi tisa za mwisho timu hizo kukutana kwenye michezo ya Ligi Kuu huku Chelsea nayo ikionekana na rekodi nzuri ya kutopoteza michezo 28 ya ligi iliyocheza ndani ya mwezi August na Mourinho ameonekana kuwa na bahati kwa kushinda mechi mechi saba kati ya 12 alizokutana na Man City inayofundishwa na kocha Pellegrini’,s huku akipoteza mbili pekee.
Vijana wa kocha Manuel Pellegrini’s niwazi watacheza kwa nguvu mchezo huo ili kutaka kushinda na kuonyesha kwamba walistaili kuwa mabingwa msimu uliopita licha ya kuzidiwa kwa idadi ndogo ya pointi na kikosi cha Mourinho.
Kiungo Muivory Coast Yaya Toure aliyefunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya West Brom Jumatatu iliyopita ataendelea kupambana kwenye eneo la kiungo huku furaha pekee kwa kocha Pellegrini ni kuimarika kwa mshambuliaji wake tegemeo Kun Aguero.
Pellegrini bado atakuwa akiwajaribu wachezaji wake wapya Rahim Sterling aliyemsajili majira haya ya kiangazi kutoka Livarpool pamoja na Wilfred Bony aliyetua kwenye dirisha dogo msimu uliopita ili kujenga ushirikiano mzuri na kikosi ambacho anadhani kitampa taji la kwanza na kuweka hai kibarua chake.
Bony na Sterling walionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo uliopita dhidi ya West Brom na kuchangia ushindi huo lakini uwezo wa Chelsea haufanani na ule wa Brom hivyo niwazi mchezo huo utakuwa mgumu na wenye mtihani mkubwa kwa kocha Pellegrini’s ambaye katika mchezo huo pia atakuwa anahitaji ulinzi imara kutoka kwa nahodha wake Vicent Company na kipa Joh Harty kuweza kuwazuia washambuliaji wa Chelsea akina Eden Hazard na Diego Coast wasiweze kuvuruga rekodi yake.
Kuelekea mchezo hou ambao umevuta hisia za wapenda soka kila kona ya dunia tayari kocha Pellegrini;s amesema kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwa anawasiwasi na kibarua chake endapo atashindwa kuchukua taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.
Kwaupande wake kocha Jose Mourinho aliyeonekana kutopendezwa na matokeo ya 2-2 na Swansea City na kupelekea kumtimua Daktari wa timu hiyo Eva Carneiro kwa madai ndiye aliyechangia timu yake kupata matokeo hayo amesema anakwenda Etihad kupata kutafuta ushindi na siyo sare au kupoteza mchezo.
Mourinho amesema anajua mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na matokeo ya mchezo wao wa kwanza na kucheza ugenini lakini watapambana kwa dakika zote 90 kutafuta pointi tatu ambazo anaamini zitawasaidia kurudisha akili zao kwenye ushindani wa kutetea ubingwa wao.
Katika mchezo huo wa Jumapili Mourinho atamkosa kipa wake chaguo la kwanza Thibaut Courtois aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 52 kwenye mchezo wa Jumapili iliyopita baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Swansea City Bafetimbi Gomis.
Kukosekana kwa Courtois niwazi Mourinho atampanga kwa mara ya kwanza kipa aliyemsajili hivi karibuni kutoka Stoke City Asmir Begovic, katika mchezo huo wa Jumapili dhidi ya Manchester City.
Ingawa Mreno huyo amesema atakata furaa kupiga adhabu hiyo aliyopewa kipa wake chaguo la kwanza lakini bado atakuwa na mtihani mkubwa kuhakikisha timu yake inacheza vizuri ugenini na kupata ushindi ikiwa ugenini licha ya kupata wakati mgumu kwa timu hiyo kila inapokutana na City.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe