Friday, July 17, 2015


Mugiraneza kutoka APR amesema, amemtazama Niyonzima wa Yanga ambaye kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ ni pacha wake wakicheza kiungo namba 6 na 8 na kuona amefanikiwa mno kisoka na kimaisha na kuamua kujaribu bahati yake Tanzania.

MAFANIKIO ya Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, kumbe ndiyo yaliyomvutia, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kiasi kufanya maamuzi ya fasta kujiunga na Azam FC atakayosaini nayo mkataba wa miaka miwili mara tu atakaporudi kutoka jijini Tanga walipoenda Ijumaa iliyopita.
Mugiraneza kutoka APR amesema, amemtazama Niyonzima wa Yanga ambaye kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ ni pacha wake wakicheza kiungo namba 6 na 8 na kuona amefanikiwa mno kisoka na kimaisha na kuamua kujaribu bahati yake Tanzania.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mugiraneza ambaye awali Yanga ilimtaka lakini aliwatolea nje, alisema: “Unajua nimemwangalia Niyonzima ambaye alikuwa pacha wangu APR na mpaka sasa kwenye timu ya Taifa, baada ya kuondoka amefanikiwa na anaporudi nyumbani Rwanda anaheshimika, ndiyo na mimi nikaamua nisifanye mchezo.
“Unajua awali, timu zilinifuata lakini kwa sababu ya utoto nilikataa, lakini sasa ni mtu mzima hivyo nahitaji changamoto nyingine ili nifikishe malengo yangu.”
Mugiraneza anatarajiwa kutumiwa na kocha Stewart Hall katika nafasi ya kiungo mkabaji na anamjaribu kwenye beki ya kati.
Mugiraneza amekwenda mbali na kusema, kutokana na mazingira aliyoyaona kwenye kikosi cha Azam, anaamini atatimiza ndoto zake.
“Azam ni timu kubwa, wana kila kitu, kama uwanja mzuri, gym, bwawa na mambo mengine mengi. Nikiwa makini nitafaidika,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe