
Hehehehe! heheheeeeee acha nicheke mie mwana wa kizibo, mjukuu wa
mdomo wa chupa. Nimepigiwa simu na mashosti zangu eti
somo nililotoa wiki iliyopita limewasaidia, sasa hivi wanakula kitu
kamili siyo msosi wa kuungaunga.
Sasa hivi safari ikianza pamoja wanamaliza pamoja. Siyo kila siku
kuteremshiana njiani na kukuacha utembee kwa miguu, nani alikuambia
hapendi raha.
Leo nataka kuwaeleza kitu kimoja kuhusu waume zetu, unajua kuna vitu
huvifanya kwa mazoea kwa vile mkewe basi, utajijua, ufike usifike shauri
yako. Nasi tusiwachekee kwa kuwaachia watufanye watakavyo, kwa kutuacha
njiani na kutufanya tutafute njia mbadala kufika mwisho wa safari.
Kazi yetu kupinda midomo kama pindo la jamvi na kumuacha mwenzako
anamwaga mzigo kisha taratiiibu anateremka, unamuangalia tu michozi
mwaaa, mbayaaaaa eeeh.
Wewe nani kakwambia kuna mtu hulia msiba kwa kushika kichwa cha
mwenzake, kila mlia msiba hushika kichwa chake, nawe unategemea kilio
chako ulie na nani kama siyo peke yako?
Leo lazima nikupe ubunifu wa kufika mwisho wa safari, ukimuona mwenzako
kashusha mzigo nawe bado, usikubali kumuachia, lazima umwoneshe kuwa
hujafika, mshike kiuno, mrudishe mwambie mwenzio bado kabisa.
Unafikiri kupinda mdomo kunasaidia nini maji ya moto yatakukomaza bure na kukutia sugu upoteze ladha halisi ya maji ya kisima.
Nawe mwanamume hivi kweli umemuoa mwenzio hata hujali mateso yake?
Hivi kweli wanajua hali ya mwanamke katika tendo, wanajua anataka nini hasa wawapo katika kilimo cha matuta. Waswahili wanasema siku zote mchuma janga hula na wa kwao, sasa mbona janga uchume wewe nile mimi?
Hivi kweli wanajua hali ya mwanamke katika tendo, wanajua anataka nini hasa wawapo katika kilimo cha matuta. Waswahili wanasema siku zote mchuma janga hula na wa kwao, sasa mbona janga uchume wewe nile mimi?
Ni wazi hata waume zetu wapo wasiojua kama wenza wao nao wanatakiwa
wafike mwisho wa safari au kujua kama mwenzie amefika au bado. Japo mimi
ni mwanamke, lakini leo nawapasha tena mpashike sichagui sibagui siku
zote raha ya wimbo kupokeza.
Siyo uimbe peke yako mwenzio kama anaumwa jino, kazi yake kugugumia kama
kakanyagwa kwenye kidonda, najua si wanaume wote wataalamu wa mambo
fulani, wengine hujua raha ya mapenzi ni kumwaga mzigo na kuteremka juu
ya mnazi.
Lazima umsome mwenzako, hasa katika safari ya kuelekea kisiwa cha utamu
usioisha hamu. Siku zote sisi wanawake tuna aina zetu za kufurahia
safari, wapo wanaohema kama wana pumu na mwisho wa safari utasikia pumzi
zake zinakwenda kwa kasi, akitulia ujue keshafika huyo.
Mwingine hupiga kelele kama kaonewa au kumaliza maneno yote mdomoni na
akiiona pwani hukujulisha kabisa kuwa chombo karibu kitatua nanga
bandarini. Nawe hapo lazima uzidishe kasi ili kuhakikisha chombo kinatua
nanga salama.
Hii itazidisha upendo na kuwafanya wake zenu mwisho wa safari watoe
asante na si kugeuka na kukupa mgongo huku mdomo umeupinda kama pindo la
jamvi. Sifa ya mwanaume si kumlisha mkewe na kumvisha, yote huwa tisa
kumi ni pale hakimu akipanda juu ya meza ya hukumu kuhukumu kulingana na
kosa.
Siku zote mbwa wake mnyororo kamba utamuonea. Siyo kaiba kuku umfunge
miaka kumi na mwizi wa ng’ombe wiki moja, usimuonee huruma katenda kosa
hilo akitegemea hukumu stahiki.
Usimuache mkeo njiani, ona aibu mwanaume usiyemfikisha mkeo unamuacha
nani amfikishe au unamlazimisha atafute wa nje? Jisikie fahari mwisho wa
safari mkeo akuambie mpenzi hakika leo umejua kunipa raha zisizo mfano.
Ni hayo
0 comments:
Post a Comment