Thursday, August 14, 2014


RAIS wa Shirikisho la Filamu Bongo ‘TAFF,’ Simon Mwakifwamba amewabwatukia wasanii wanaodai  shirikisho hilo limeanguka baada ya baadhi yao kujiunga na Bongo Movie Unity.

RAIS wa Shirikisho la Filamu Bongo ‘TAFF,’ Simon Mwakifwamba.
Akizungumza kwa hisia kali na gazeti hili, Mwakifwamba alisema, TAFF ni taasisi kubwa na ipo kwa ajili ya kushughulikia mambo yenye tija kwenye tasnia ya filamu na haipo kwa ajili ya umaarufu kwani kila mtu ni maarufu hivyo anamshangaa Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kusema iko chali.
“Sisi siyo watu wa matukio kama harusi bali tupo kwa ajili ya kutetea masilahi ya wasanii, ni kituko sana mtu kutufananisha na Bongo Movie Unity.
“Nawashangaa wanaosema wasanii maarufu wametukimbia, sisi hatupo kwa ajili ya umaarufu. Hatujashindwa kulipia kodi ya ofisi yetu wala umeme sasa tukoje chali wakati mambo yanaenda vizuri?” alihoji Mwakifwamba.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe