Sunday, July 27, 2014

Mratibu wa Semina hiyo ambaye ni Marketing and Customer Service Manager wa GEPF,  Aloyce Ntukamazina akizungumza na wasanii.

Wasanii wakifuatilia kwa ukaribu maelekezo.
Hapa msanii Cloud na Simon Mwapagata wakiuliza maswali.
.....semina ikiendelea.
Baadhi ya wasanii wakielekezwa kujaza fomu za GEPF
Hapa wakihojiwa na mwandishi wa Global TV Online.
Wasanii wa filamu na muziki Bongo wamepigwa semina na wataalamu wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kupitia mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ya uzeeni.
Semina hiyo iliyokwenda sambamba na futari yenye malengo, ilifanyika jana jioni katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo jijini Dar.Akizungumza na wasanii hao Mratibu wa Semina hiyo
ambaye ni Marketing and Customer Service Manager wa GEPF,  Aloyce Ntukamazina alisema kuwa wasanii hao hawana budi kujiunga na mfuko huo kwa sababu una masharti nafuu kuliko mfuko wowote nchini.
Semina hiyo iliisha kwa wasanii hao kufuturu kwa pamoja kisha wote kujiunga na mfuko huo na kukabidhiwa vitambulisho.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe