Rais
Jakaya Kikwete akiwa na mpira tayari kuanzisha mechi ya wabunge wa
Simba na Yanga wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, mwaka huu
linafanyika Agosti 8.
LILE tamasha lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki,
linalotambulika kama Usiku wa Matumaini (Night of Hope), limewadia
ambapo mwaka huu litafanyika Agosti 8 (Sikukuu ya Nanenane.)
Mashabiki wa timu ya Bongo Muvi wakiingia uwanjani kwa mbwembwe kabla ya timu yao kumenyana na Bongo Fleva mwaka jana.
Akizungumza na Mtandao huu, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto
amesema mwaka huu wamelifanyia maboresho ya hali ya juu kutokana na
kuchukua wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki ili kukata kiu ya
Watanzania ambao walitoa maoni na kupendekeza aina ya wanamuziki na
burudani wanazopenda ziwepo.
“Historia itaandikwa upya na kwamba Watanzania wakae tayari kuisubiri
Agosti 8, mwaka huu, muda si mrefu tutaanza kutaja orodha kamili ya
wasanii wakubwa tutakaokuwa nao ambao kwa hakika itakuwa ni sapraizi kwa
mashabiki wa burudani Bongo,” alisema Maloto na kuongeza:
Dk. Jose Chameleone akifanya yake katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2012.
“Kama kawaida, Tamasha la Usiku wa Matumaini litafanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ule mpya, mkubwa.”
Tamasha la Usiku wa Matumaini huandaliwa na Kampuni ya Global
Publishers, ambapo linachukua nafasi kila mwaka na linawakutanisha watu
wengi kutokana na matukio mbalimbali yanayolipamba tamasha hilo.
Benchi la timu ya Wabunge wa Simba.
Miongoni mwa matukio ambayo yalisisimua mwaka jana kwenye tamasha
hilo ni pamoja na mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge, ndondi za
wabunge, mechi za Bongo Fleva na Bongo Movie, bendi mbalimbali
kutumbuiza pamoja, mastaa mbalimbali wa muziki wa Gospo kutoka ndani na
nje ya Bongo.
0 comments:
Post a Comment