MASTRAIKA wa Yanga, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi na Hamis
Kiiza, wamemfanya kocha Mbrazili Marcio Maximo kushindwa kusajili fowadi
mpya.
Okwi na Kiiza bado hawajaripoti kwenye mazoezi ya
Maximo na wapo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’
inayojiandaa na mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
dhidi ya Mauritania.
Maximo aliliambia Mwanaspoti: “Nimekuwa na
mapendekezo mengi ambayo nimepeleka kwa viongozi wa klabu likiwemo la
kuleta mastraika wapya, lakini hilo limekwama kwa sasa mpaka pale kina
Okwi na Kiiza watakapowasili.
“Wakishawasili nitahitaji kuwafanyia uchunguzi wa
umakini ili nibaini iwapo nitahitaji straika mpya au nitajitosheleza
nikiwa nao.” Alisisitiza kwamba ana mipango ya kuifanya Yanga kuwa klabu
ya kimataifa na ambayo itajitangaza yenyewe ikiwa inaigwa na wengi.
“Sitaki kusema kuwa na sisi tunataka kuwa kama klabu za TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yenye kusifika kwa utajiri. Sisi Yanga
tunataka kuwa kama Yanga kwenye soka la Afrika.
“Nataka kuiendeleza Yanga nje na ndani ya uwanja
kwakuwa wanachofanya viongozi na mashabiki kinahitaji kuifanya Yanga
kuwa ya kipekee na ya kimataifa.
“Hisia za watu mitaani zinanifanya niamini kuwa
Yanga inatakiwa kuwa ya kiprofesheno, pia Yanga yenye nidhamu ya hali ya
juu na pia yenye kuleta ushindani nje na ndani ya nchi.”
Wiki hii Maximo alifanya uamuzi mgumu kwenye
kikosi cha Yanga baada ya kuwarejesha kundini Abuu Ubwa na Hamis Thabiti
waliokuwa wametemwa kwenye kikosi hicho kwa nyakati tofauti ambapo jana
Ijumaa alilitolea ufafanuzi suala hilo.
Maximo alisema: “Nina jukumu la kuwaweka vizuri
wale vijana waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa chini ya miaka 17
wakati nikiwa na Taifa Stars ambao kwa sasa wameonekana kupotea na pia
wale wanajitahidi kupanda hususani wa timu ya vijana ya Yanga.
“Naamini wachezaji kama kina Thabiti, Ubwa wana
nafasi ya kurudisha ubora waliokuwa nao miaka minne iliyopita wakiwa
Serengeti Boys (timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ). Hii
itaisaidia Yanga kwa siku zijazo. Tayari pia nina wachezaji kama saba wa
timu ya vijana.
0 comments:
Post a Comment