Tuesday, July 8, 2014


MMOJA wa wasanii wa muda mrefu kunako Bongo Fleva, Ahmed Mohamed Kakoyi ‘Mad Ice’, ambaye kwa sasa anafanya muziki wake kimataifa zaidi, amesema anavutiwa na wasanii wa nyumbani, lakini anasikitika kwamba wengi wao wanaiga muziki wa Nigeria.

Msanii wa muda mrefu kunako Bongo Fleva, Ahmed Mohamed Kakoyi ‘Mad Ice’.
Katika mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake, Mikocheni jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mad Ice alisema mojawapo ya sababu zinazowafanya wasanii wa Nigeria kufahamika nje ni kwa sababu ya kupewa sapoti kubwa na vyomho vyao vya habari.
Yafuatayo ni baadhi ya mahojiano hayo ambayo pia yanapatikana kwa kirefu katika Global TV online, inayoonekana kupitia
Swali: Mambo vipi kaka?
Mad Ice: Poa kabisa.
Swali: Hebu tuweke sawa kidogo, mimi sielewielewi hasa wewe ni raia wa wapi?
Mad Ice: Mimi ni raia wa Uganda, lakini nimeishi sana Tanzania kiasi najiona kama raia wa hapa.
Swali: Umekuwa kimya sana siku hizi, husikiki kama zamani, tatizo nini?
Mad Ice: Nilikuwa katika harakati za kuangalia nitaliteka vipi soko la kimataifa, hata hivyo hivi sasa nimeweza kuutanua muziki wangu huko ndiyo maana naonekana kama sisikiki sana hapa nyumbani, lakini bado naendeleza makamuzi kama kawa.
Swali: Kwa nini uliamua kuoa Mzungu badala ya Mwafrika mwenzako?
Mad Ice: Mzungu na Mwafrika wote ni binadamu, sioni tatizo, mbona Wazungu nao wanaoa Waafrika, kawaida tu.
Msanii Linex.
Swali: Vipi kuhusu filamu za hapa nyumbani, umewahi kuziangalia? Kama ndiyo msanii gani anakuvutia?
Mad Ice: Huwa naziangalia lakini kusema kweli filamu za Kibongo hazina ubunifu wala maandalizi ya kutosha, filamu moja tu ndiyo niliweza kuangalia mwanzo mwisho na hiyo ilikuwa ni ile ya  Girl Friend iliyoongozwa na marehemu George Otieno ‘Tyson’.
Swali: Vipi kuhusiana na siasa, unafuatilia siasa za ukanda huu wa Afrika Mashariki?
Mad Ice: Zamani nilikuwa nafuatilia lakini kwa sasa nazichukia kupita maelezo kwa sababu zimejaa ubabaishaji hususan kwa nchi zote za kiafrika,  viongozi walio wengi wamejaa tamaa, wana uchu wa  kujilimbikizia mali bila ya kujali matatizo ya wananchi wao.
Swali: Kwa hapa nyumbani, ni msanii gani anakuvutia zaidi kusikiliza kazi zake?
Mad Ice: Hahahaa; Nawakubali wengi lakini kuna baadhi ambao wananikosha sana ninaposikiliza muziki wao, kwa mfano bwana mdogo Linex na AT, aina ya muziki wao huwa naipenda, wanajitahidi kusema kweli hivyo waongeze bidii wasibweteke na hapo walipofikia, ikiwezekana nao wajitanue zaidi kimataifa.
Swali: Familia yako ina watoto wangapi?
Mad Ice: Nina watoto watatu ila kwa sababu ninazozijua mwenyewe, siwezi kutaja majina yao.
Swali: Umefanya muziki kwa muda mrefu, je una mafanikio gani?
Mad Ice: Nimepata mafanikio mengi, lakini pia nimeweza kutembelea nchi nyingi duniani kwa kufanya shoo na kujua mambo.
Swali: Nini tofauti kati ya Mad Ice wa sasa na yule wa zamani?
Mad Ice: Mad Ice wa sasa amejikita kimataifa zaidi kwa kutangaza muziki wake na kufanya shoo za katika majukwaa ya kimataifa.
Swali: Mbali na muziki unajishugulisha na nini?
Mad Ice: Nina kampuni yangu, pia nina studio ya kutengeneza muziki na mambo mengine kibao.
Swali: Una mpango gani kuwasaidia chipukizi ili nao siku moja wafike ulipofikia?
Mad Ice: Nina mipango endelevu kwa chipukizi wanaojitambua, lakini nisingependa wale ada za shule kwa ajili ya muziki.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe