Wednesday, July 16, 2014

KUPENDA ni hisia za ndani. Hata siku moja, mtu hawezi kulazimisha kupenda. Ni mpaka moyo wake uamue wenyewe. Wakati fulani hisia hizo hutoweka.

Kwa bahati mbaya ni kwamba, wakati hisia za kupenda na msisimko wa mapenzi vikiondoka, mhusika huwa hana taarifa. Ni wachache sana hujigundua.
Wengi hujikuta tu– tena wenzi wao ndiyo hugundua mapema na huathiriwa na mabadiliko hayo kuliko wahusika wenyewe.
Hata hivyo hao wachache wanaobahatika kujua wapo kwenye tatizo hilo huwa ni wagumu sana kuwaeleza ukweli wenzi kuhusiana na matatizo yao. Sababu hiyo huwafanya wengi kuingia kwenye migogoro isiyo ya lazima na wenzi wao.
Hapa kwenye All About Love nitakusaidia namna ya kumrejesha mwenzi wako aliyepoteza msisimko na hisia za kupenda.
Hiyo itakusaidia kujenga upya penzi lenu ambalo liliporomoka au limeanza lakini ukagundua kuwa linaweza kwenda bila kuwa na nguvu ya kutosha. Je, utawezaje kumgundua aliyepoteza hisia za kupenda? Twende pamoja...
NI RAHISI KUMTAMBUA
Ni afadhali uwe katika hatua za kumfuatilia, kabla hujajua chochote ukagundua wazi kwamba, huyu ana tatizo la kupenda, lakini ukishaingia katika uhusiano naye, ni vigumu sana kujua, maana unaweza kuhisi anakudharau kumbe mwenzio mgonjwa!
Lakini hapa, zipo njia za kitaalamu kabisa ambazo zinaweza kukufanya ugundue mpenzi wako ana tatizo la ugonjwa wa kupenda! Hebu tuone...
(i) Msiri
Sifa ya kwanza kabisa ni kwamba, hataki kukupa nafasi ya kumjua vizuri, anakuogopa, maana ukijua udhaifu wake unaweza kumtenda na kumfanya aishi mpweke kwa mara nyingine. Ni msiri sana, hataki ujue ratiba zake na mambo yake mengi anafanya kwa kushtukiza (huyu si kwamba anajijua kuwa ana tatizo, ila anahisi tu).
(ii) Simu yako humshtua!
Hayupo katika penzi la msisimko, kwa hiyo hata akiona simu yako anashtuka na kuogopa kupokea haraka. Hana amani ya moyo. Hapendi kukusikia ukisema; “I love you baby!” maana anahisi kama unamuumiza tu!
Kwa hiyo unaweza kumpigia simu ikaita kwa muda mrefu sana bila kupokea na hata akipokea, sauti yake huwa haina msisimko wa mahaba. Ni rahisi sana kumsikia akisema: “Nakusikiliza...ulikuwa unasemaje? au sema nakusikia..., kuna nini tena?” na kauli nyingine zinazofanana na hizo.
Kauli hiyo inatosha kabisa kukuthibitishia kwamba upo na mwenzi ambaye hana msisimko kabisa na wewe.
(iii) Mzito kukuambia anakupenda!
Ukiwa naye katika mahaba au mtoko, ukimwambia: “Nakupenda sana mpenzi wangu,” yeye anaona shida sana kukujibu anakupenda pia. Sababu kubwa hapa ni majeraha ya moyo.
Huwa anahisi kama atakuwa anakudanganya, maana moyo wake una bandeji kila kona! Hana uhakika na mapenzi yake, inawezekana akawa kweli anahisi kukupenda, lakini bado akawa hana imani sana na maneno yanayotoka kinywani mwako.
(iv) Wasiwasi mwingi
Mara zote amekuwa na wasiwasi, hapendi mkae sehemu za uwazi, anafikiria juu ya kuachwa, huku utumwa mkubwa zaidi ukiwa ataificha wapi aibu yake siku na wewe ukimwambia utamwacha.
Haamini kama anaweza kuwa mpenzi wako siku zote, kwa hiyo kuliko ‘ajichoreshe’ kwa watu kuwa yupo na wewe ni bora akae ‘nyumanyuma’ kwa hofu ya kuchekwa na kubezwa siku akiachana na wewe maana hana uhakika wa kudumu na wewe.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe