(Picha/habari: Gladness Mallya na Hamida Hassan/GPL)
Stori:Na Gladness Mallya na Hamida HassanMSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma, ameamua kutoka kivingine tofauti na filamu ambapo amefungua sehemu ya kuoshea magari ‘Car wash’ inayojulikana kwa jina la Mamii White ikiwa ni njia mojawapo ya kuendelea kujiongezea kipato.
Wastara amezindua Car wash hiyo iliyopo maeneo ya Tabata Muslim jijini Dar es Salaam ambapo watu kibao wamehudhuria na magari yao huku wakipewa ofa ya kuoshewa na kusherehekea kwa kula na kunywa na kucheza muziki.
0 comments:
Post a Comment