
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dokta Fenella Mukangara jana usiku alizindua maadhimisho ya Siku ya Msanii hapa nchini ambayo huadhimishwa Oktoba 25 kila mwaka ulimwenguni kote. Maadhimisho hayo yalifanyika kwenye Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Masaki, Jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo alisema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar, ambapo wasanii wa fani mbalimbali wakiwemo wanamuziki, wachoraji na wengineo watatunukiwa tuzo. Dokta Mukangara pia amesema serikali kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa 'Basata' ndiyo waratibu wa maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment