
FAINALI za Kombe la Dunia zimeanza Juni 12, mashabiki wamekuwa wakifuatilia fainali hizo kwa mtazamo wa hali ya juu.
Chini kuna dondoo za mambo yaliyotokea siku ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne na ya tano, tazama yapo mengi lakini haya ni baadhi tu.
Siku ya kwanza
Usivuke mstari
Waamuzi waliibuka kivutio kwa kuanza kuchora sehemu mpira unapowekwa kama ni faulo inapigwa, lakini pia sehemu ukuta unapowekwa ili wasivuke, hii ilikuwa kivutio kwa kuwa wizi hakuna tena.
Achana na mbio za Oscar.
Pamoja na kwamba alikuwa staa kwenye mchezo wa kwanza kati ya Brazil na Croatia, lakini Oscar wa Brazil alivutia zaidi kwenye bao la tatu alilofunga baada ya kukimbia na kufunga kiufundi zaidi.
Uwanja kimya!
Awali mashabiki wa Brazil waliamini kuwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza ni haki yao lakini baada ya kuwa nyuma mapema tu kipindi cha kwanza, mashabiki walitulia kimya na kuwaacha Croatia wachache ‘wakishaini’, hata hivyo walishinda 3-1.
Siku ya pili
Fainali ya Kombe la Dunia iliendelea tena siku ya pili na hapa ndipo utamu ulipokolea zaidi kwani kulikuwa na mechi nyingi ambazo zilikuwa na mvuto.
Chile ni kiboko
Awali walikuwa hawapewi nafasi kubwa sana ya kufanya maajabu kwenye fainali hizi, lakini walishangaza baada ya kuwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Australia na mwisho kuibuka na ushindi.
Robben alipa kisasi
Baada ya kukosa nafasi kadhaa za wazi kwenye fainali ya mwaka 2010, Arjen Robben wa Uholanzi, alirejea kwenye mchezo wao dhidi ya Hispania na kufanya kazi ya hali ya juu, alifanikiwa kufunga mabao mawili, Robin van Persie mawili, huku timu yao ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1.
Kazi mbovu ya waamuzi
Siyo kwamba tu fainali za mwaka huu zilikuwa bora, bali waamuzi nao walifanya yao siku ya pili baada ya kukataa mabao ambayo dhahiri yalionekana kuwa sahihi kwenye mchezo kati ya Mexico na Cameroon. Lakini pia kuna swali kwenye penalti ya Hispania dhidi ya Uholanzi.
Mholanzi aliyepaa
Kama wataalamu wameanza kutafuta bao la msimu, basi lile la Robin van Persie dhidi ya Hispania lipo pale juu huku mengine yakifuata kwa chini.
Mshambuliaji huyo alipaa kama ndege na kufunga bao safi la kusawazisha kwa kichwa akipata mpira wa umbali wa mita 51.
Siku ya tatu
Hii ilikuwa siku pekee ambayo fainali za Kombe la Dunia zilishuhudia michezo minne, katika michezo hiyo, mashabiki walishuhudia mabao 13 yakitinga wavuni.

Kiboko yao ni Pirlo
Halikuwa bao lakini faulo iliyopigwa na kiungo babu wa Italia, Andrea Pirlo, ilitosha kuwaamsha mashabiki wote waliokuwa wamelala baada ya kugonga mwamba huku kipa wa England, Joe Hart, akiwa hana la kufanya, achana na hizo pasi zake ndani ya dakika tisini, zilikuwa bora sana.
Colombia wafunga kazi
Mashabiki wengi walikuwa wanasubiri kuwaona Ghana jinsi watakavyoshangilia endapo watafunga bao, lakini shangilia ya Colombia imewafuta kiu yao.
Bao la Pablo Armero, alilofunga dhidi ya Ugiriki lilikuwa bora sana, lakini shangilia yao nayo ilikuwa bora zaidi.
Nani atanitibia?
Hili linaweza kuwa swali alilouliza daktari wa England baada ya kudondoka wakati akishangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Daniel Sturridge, hata hivyo walilala kwa mabao 2-1.
Kizazi cha ushindi
Dakika mbili zilitosha kuwapa Ivory Coast ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo dhidi ya Japan, Ivory Coast walianza kuwa nyuma lakini mabao ya Bony na Gervinho dakika ya 64 na 66 yaliwapa ushindi wa mabao 2-1.
Siku ya nne
Siku hii pia ilikuwa bora kwa mashabiki kushangilia mabao, yalifungwa mabao tisa kwenye michezo mitatu, ilikuwa siku nyingine ya mvuto kwa Kombe la Dunia.
Ilikuwa siku ambayo mashabiki waliona kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi, chini kuna dondoo za siku hiyo:
Benzema ni habari nyingine:
Benzema alifanya kazi kubwa sana kwenye mchezo wa kwanza wa Ufaransa dhidi ya Honduras, alifunga mabao mawili, alitengeneza la tatu la kujifunga, angeweza hata kufunga matano kama angekuwa makini.
Teknolojia yamchanganya mwamuzi
Bao la tatu la Ufaransa lilikuwa na utata baada ya mwamuzi na teknolojia ya kutambua kama mpira umeingia au la kupishana. Hata hivyo, mwamuzi aliamuru ni bao baada ya kujadiliana na mwenzake.
Messi afufuka
Mashabiki wengi hawakuamini kama mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi, anaweza kuibeba timu yake, lakini ushindi wa mabao 2-1 waliopata dhidi ya Bosnia na Herzegovina, Messi anahusika kwa asilimia kubwa.
Siku ya tano
Siku hii kulikuwa na mechi ngumu kadhaa, Nigeria na Ghana waliingia uwanjani kwa mara ya kwanza na wote waliambulia sare.
Lakini ukiacha hapo, kumbuka Ureno walikutana na kichapo kikali toka kwa Ujerumani.
Nigeria wakongwe nje…
Mashabiki wa Nigeria wameonyesha kukasirishwa na kitendo cha kocha Stephen Keshi, kuwaweka nje wachezaji wengi wazoefu na kuwaanzisha wengi chipukizi, hata hivyo timu yao iliambulia sare ya bila kufungana na Iran.
Mwenye kiatu chake arejea
Mshambuliaji aliyetwaa kiatu cha dhahabu mwaka 2010 nchini Ujerumani Thomas Mueller alianza kazi yake ya kuwania kiatu hicho tena baada ya kufunga mabao matatu kweney ushindi wa 4-0 ambao timu yake ilipata dhidi ya Ureno. Bado anaonekana kuwa anaweza kukichukua tena.
Lakini pigo lilikuwa kwa Cristiano Ronaldo aliyetoka uwanjani kichwa chini.
Bao la mapema
Hata kabla mwamuzi hajatoa filimbi mdomoni mshambuliaji wa Marekani Clint Dempsey, alishaifungia timu yake kwenye sare ya 2-1 dhidi ya Ghana, hii ilikuwa sekunde ya 32 na kuwa bao la mapema zaidi kwenye Kombe la Dunia.
Siku ya tatu
Hii ilikuwa siku pekee ambayo fainali za Kombe la Dunia zilishuhudia michezo minne, katika...
Siku ya nne
Siku hii pia ilikuwa bora kwa mashabiki kushangilia mabao, yalifungwa mabao tisa kwenye michezo...
0 comments:
Post a Comment