Coutinho akiwa katika pozi.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mohammed Binda (kushoto), akiwa akiwa na Coutinho baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Msemaji
wa Yanga, Baraka Kizuguto (wa tatu kutoka kushoto) akimuongoza mchezaji
huyo baada ya kumpokea uwanjani hapo. Wengine ni mashabiki wa Yanga
waliofika uwanjani hapo kukipokea ‘kifaa hicho’.
KIUNGO mshambuliaji raia wa Brazil, Andrey
Coutinho leo ametua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) jijini Dar es Salaam tayari kwa kukipiga kwenye timu ya Yanga ya
Dar es Salaam. Mchezaji huyo alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Yanga
akiwemo msemaji wa timu hiyo, Baraka Kizuguto.
0 comments:
Post a Comment