
KOMEDIANI maarufu Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ alijikuta akipagawishwa vilivyo na shoo ya Malkia wa Taarab Bongo, Khadija Kopa kiasi cha kushindwa kujizuia na kupanda jukwaani kuungana na wacheza shoo wake.

Mboto akiwa jukwaani alishangiliwa sana, aliposhuka aliwekwa kati na gazeti hili ambapo alisema: “Namkubali sana Khadija Kopa, kiukweli nilivutiwa na kipande alichoimba kwenye wimbo wa Tulinde Utanzania, ndiyo maana sikuona haja ya kujivunga.”
0 comments:
Post a Comment