MWANAMITINDO Jokate
Mwegelo ameibuka na ubunifu mpya wa sabuni ya kuogea inayokwenda kwa
jina la Mo hiyo ikiwa ni baada ya kutesa na bidhaa ya ndala.
Akipiga
stori na Risasi Mchanganyiko, Jokate alisema uzinduzi wa sabuni hiyo
unatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Juni 18, mwaka huu ambapo yeye na
timu yake watatembea kwa miguu kutokea mjini (Posta) kuelekea Mbagala
huku wakigawa zawadi kwa a kina mama.
“Nashukuru
nimeweza kubuni tena bidhaa nyingine, nataka kuwaambia wasichana
wenzangu, wasilale. Tukitaka tunaweza kufanya makubwa. Nawashauri
wapenzi wangu wakae barabarani kunisubiria nitapita na kundi langu la
Kidoti ili niwapatie zawadi,” alisema Jokate.
0 comments:
Post a Comment