
Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”
Rais
Jakaya Kikwete akimpa mkono wa pongezi msanii mkali katika miondoko ya
Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' kwa hatua aliyofikia.
Diamond (kushoto) akiwa na mkali mwingine wa muziki kutoka Nigeria, maarufu kwa jina la Davido (aliye mbele pichani).“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete.
Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani hatapata chochote.
RSS Feed
Twitter
12:33 PM
Unknown

Posted in
0 comments:
Post a Comment