Stori: Mwandishi WetuHUKU ajali za barabarani zikizidi kuongezeka kila siku hasa jijini Dar es Salaam, timu ya uchunguzi ya Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, hivi karibuni lilifanikiwa kuyanasa baadhi ya magari kadhaa yanayokiuka sheria za usalama barabarani.
Magari hayo, ambayo yalikuwa kinara wakati wa uchunguzi huo, yakiwemo yenye namba za usajili zinazoonyesha kuwa ni kutoka idara mbalimbali za serikali, yalikutwa yakiendeshwa kwa kasi maeneo yasiyoruhusiwa, yakitanua kinyume na utaratibu na wakati mwingine yakipita katika makutano ya barabara, licha ya taa nyekundu kuwaka.
Katika baadhi ya makutano ya barabara kama vile Tazara, Bamaga na Ubungo, magari hayo, ambayo baadhi yao yanaonekana katika ukurasa wa mwisho wa gazeti hili, yalipita kwa mwendo kasi licha ya kuzuiwa na taa, hali ambayo inaleta uwezekano mkubwa wa ajali.
OMF lilishuhudia gari lenye namba za usajili T 896 BQQ baada ya kuvuka huku taa nyekundu zikiwaka, almanusura limgonge mtembea kwa mguu aliyekuwa akivuka katika makutano ya barabara ya Bamaga, Mwenge wilayani Kinondoni.
Gari
hilo lilitokea Mwenge likiwa katika mwendo wa kasi na halikujali kama
taa nyekundu zilikuwa zikiwaka (kuashiria lisipite) na magari mengine
yanayotokea Sinza kuelekea Sayansi yalikuwa yanapita.
Uchunguzi
umebaini kuwa vitendo hivi vya ukiukwaji wa sheria za usalama
barabarani hufanyika zaidi wakati askari wakiwa hawapo maeneo hayo,
lakini madereva hao huzingatia sana sheria endapo trafiki wakiwa eneo la
tukio.
OFM
inaendelea na kampeni ya kuyabaini magari yote yanayokwenda kinyume cha
sheria za usalama barabarani na kitayafikisha magari yote kwa Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga kwa hatua zaidi.Aidha kwakuwa magari mengi ya daladala pia yamo, OFM itayafikisha kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri nchi kavu na majini (Sumatra) Ahmed Kilima.
RSS Feed
Twitter
1:22 PM
Unknown


Posted in
0 comments:
Post a Comment