ENGLAND imepoteza mechi ya pili mfululizo ya Kundi D Kombe la Dunia, baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Uruguay mjini Sao Paulo, Brazil.
Mbaya wa England alikuwa mshambuliaji wa
Liverpool, Luis Suarez aliyefunga mabao yote mawili, moja kila kipindi
wakati bao pekee la England limefungwa na mshambuliaji wa Manchester
United, Wayne Rooney.
Uruguay walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 39, baada ya Luis Suarez kumalizia kazi nzuri ya Cavani.
England walisawazisha dakika ya 75, Wayne Rooney akimalizia vizuri krosi ya Glen Johnsont.
Bao hilo liliwapa tamaa ya mabao zaidi England na kujikuta wanamsahau kidogo Suarez, ambaye alitumia mwanya huo kuwafunga bao la pili dakika ya 85.
Suarez alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira mrefu wa juu uliomshinda Nahodha wa England, Steven Gerrard na kumtungua Joe Hart.
Kikosi cha Uruguay kilikuwa: Muslera, Gimenez, Godin, Caceres, Pereira/Fucile dk79, Lodeiro/Stuani dk67, Gonzalez, Arevalo Rios, Rodriguez, Cavani na Suarez/Coates dk89.
England: Hart, Baines, Cahill, Jagielka, Johnson, Gerrard, Henderson, Sterling/Barkley dk64, Rooney, Welbeck/Lallana dk71 na Sturridge.

0 comments:
Post a Comment