Saturday, June 7, 2014

ASHA BARAKA: SITAMSAMEHE CHOKI

Stori: Paparazi Wetu
MKURUGENZI wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka, amesema kamwe hawezi kumsamehe mwanamuziki Ally Choki ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, ambaye ana bifu naye la muda mrefu.
Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka akifunguka jambo katika ofisi za Global Publishers, zilizopo Bamaga Mwenge.
Hivi karibuni habari zilienea kuwa wawili hao wameshapatana baada ya kukutanishwa na chombo kimoja cha habari nchini, jambo ambalo Asha amelikanusha.
“Siwezi kupatana na Choki kwa sababu sioni haja ya kufanya hivyo. Nimesikia kwenye mitandao kuwa eti tumepatanishwa... watu bwana! Labda waliopatana ni wao siyo mimi. Nasisitiza habari hizo ni za uongo na ninaomba Choki akae mbali na mimi,” alisema Asha.
Ali Choki ndani ya ofisi za Global Publishers.
Kwa upande wa Choki, alipoelezwa kuhusiana na majibu ya Asha, alicheka kisha akasema: “Kama yeye amesema hivyo, acha iwe hivyohivyo. Kwanza hayo mapatano yenyewe sijafanya kwa ajili yake maana hakuna kitu ninachotaka kwake. Nina mambo mengi ya kufanya.”

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe