MAKOCHA kutoka nchi mbili za Brazil na Uholanzi ndiyo wenye nafasi ya kuifundisha Yanga msimu ujao.
Habari za uhakika kutoka Yanga zinaeleza, Yanga inataka kupata kocha Mholanzi ili kuendeleza utamaduni wa Kiholanzi baada ya kufundishwa na Ernie Brandts na Hans van der Pluijm.
Lakini kama mambo hayataenda vizuri itaangalia nchi nyingine na Brazil ndiyo inapewa nafasi kuwa ya pili katika hilo.
Mmoja wa viongozi wa Yanga ameliambia Championi Jumatatu kuwa viongozi wamekuwa wakifanya juhudi kubwa kupata kocha wa kuaminika.
“Lazima awe kocha wa kuaminika na mwenye heshima kubwa, mambo hayawezi kwenda kirahisi na itakuwa kazi lakini lazima tuwe na kocha wa uhakika.
“Mawasiliano kila sehemu yanaendelea na Brazil ni sehemu moja ambayo tunahitaji kupata kocha kwa kuwa wako wengi mahiri,” kilieleza chanzo.
Lakini taarifa nyingine zinaeleza, Pluijm pia ameanza mawasiliano na kocha raia wa Uholanzi na huenda akatua nchini hivi karibuni.
Pluijm ambaye ametua nchi leo alfajiri akitokea Saudi Arabia alipokwenda kusaini mkataba na klabu yake mpya, ataondoka kesho au keshokutwa kwenda Ghana kusaka wachezaji wawili kwa ajili ya Yanga na atakuwa akiendelea na suala hilo la kocha.
0 comments:
Post a Comment