Thursday, May 8, 2014

WANAFUNZI WAULA SHINDANO LA FUMBO MASHULENI

Mkurungezi wa Unilever Raymond Banda akizungumza na waandishi wa habari katika Hotel ya Serena Jijini kwenye Uzinduzi wa Shindano la Fumbo mashuleni.

Wanafunzi wakifwatila kwa umakini.
Wafanyakazi wa Unilever Tanzania.
Wanafunzi wakitazama kwenye Ubao ambao utatumika kubandikia Tokeni za ushindi.
Kamishna wa Wizara ya Elimu Tanzania, Dokta Leticia Sayi akizindua shindano la Fumbo mashuleni.
Raymond Banda akimskiliza Mgeni rasmi.
Leticia Sayi akiongea jambo.
Bidhaa za Unilever Tanzania zikionyeshwa.
Wanafunzi wakifwatila maelezo.
Stori : Deogratius Mongela
SHULE 600 pamoja na Wanafunzi laki tano wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea kitita cha Shilingi millioni 19 kwa Shule itakayoshinda pamoja na  Wanafunzi wawili wakipelekwa Marekani kujifunza zaidi kupita kampuni ya Unilever Tanzania chini ya bidhaa yake ya blue band.
Akifungua Shindano hilo  katika Hotel ya Serena  Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa Habari   Kamishna wa Wizara ya Elimu Tanzania Dokta Leticia Sayi amewapongeza sana kampuni hiyo kwa kuanzisha Shindano kwa Shule zote za hapa nchini na kutoa nafasi kwa wanafunzi wote kushiriki kikamilifuna kuongeza ufanisi wao wakati wa kiwa Mashuleni.
Mkurungenzi wa kampuni hiyo, Raymond Banda  alisema Dhamira yao ni kuendelea kutoa bidhaa bora zaidi kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani zikiwa kwenye kiwango cha juu kwa ubora na kudumisha Afya, uzito wa Mwili , pamoja na nafasi ya watoto kutopatwa na magonjwa madogo madogo wakiwa wanapata lishe bora ndiyo maana wanasisitiza Blue band mashuleni .

Shindano hilo litahusisha shule za msingi zaidi ya 600 katika maeneo yote ya nchi ambapo Wanafunzi 500,000 na Walimu 600, watania zawadi  Shindano litaanza Mwezi Mei hadi Agosti mwaka huu, huku washindi wakitarajia kunyakua milioni 190 na  watakaofanya vizuri katika Shindano hilo watapata nafasi ya Kwenda Marekani akiambatana na Mzazi mmoja kwa lengo la kujifunza zaidi.
Picha na Stori: Deogratius Mongela

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe