
Kabla ya kugombana Nemanja Vidic wakiwa na Evra katika furaha
MABEKI wa Manchester United, Nemanja Vidic na Patrice Evra,
wameripotiwa kukunjana mashati kabla ya kocha David Moyes kuwagombelezea
wakati walipotaka kuzipiga mazoezini kwa hasira zinazotokana na timu
kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu England msimu uliomalizika hivi karibuni.
Mastaa hao wameripotiwa kutaka kuzipiga baada ya
timu yao kuchapwa 3-0 na Liverpool kwenye Ligi Kuu England uwanjani Old
Trafford Machi mwaka huu na hivyo kutibua zaidi msimu wao kabla ya kocha
Moyes hajatimuliwa na Ryan Giggs kuchukua mikoba.
Kwenye mchezo huo ambao Vidic, alitolewa kwa kadi
nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano na mwamuzi, Mark
Clattenburg, alimshutumu Evra kwa kushindwa majukumu yake ya ulinzi
kwenye mechi hiyo na kusababisha beki ya Man United kuonekana dhaifu
wakati wa mchezo.
Kauli hiyo imeelezwa ilimtibua Evra na kukunjana
mashati na beki mwenzake, kabla ya kocha wao kuingilia kati kuwapangua
kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo huko Carrington.
Vidic anaondoka Old Trafford na kwenda kujiunga na Inter Milan baada ya miaka minane aliyodumu Man United.
0 comments:
Post a Comment