Na Hans Mloli
MIKAKATI mingi katika kipindi hiki cha usajili mkali na wa umakini zaidi kwa ajili ya msimu ujao inaendele na sasa Simba wamekubaliana kutofanya tena usajili wa gharama wa mamilioni ya shilingi kutokana na sababu mbalimbali.
Mpaka sasa Simba haijafanya usajili wa mchezaji yeyote zaidi ya
kuwatema baadhi ya wachezaji wao huku ikielezwa kuwa, lengo lao ni
kufanya usajili wa siri mno na wa kushtukiza bila ya kuingia kwenye
mvutano na timu yoyote ile.MIKAKATI mingi katika kipindi hiki cha usajili mkali na wa umakini zaidi kwa ajili ya msimu ujao inaendele na sasa Simba wamekubaliana kutofanya tena usajili wa gharama wa mamilioni ya shilingi kutokana na sababu mbalimbali.
Imeelezwa kuwa Simba waliweka kikao kwa ajili ya mjadala huo wa usajili hivi karibuni na wakakubaliana baadhi ya mambo, la kwanza likiwa ni kutosajili mchezaji yeyote wa Yanga lakini la pili ambalo lilikuwa bado lipo nyeti ni kutotumia mamilioni kusajili wachezaji kwa kuwa tathmini inawaonyesha kwamba wachezaji wengi waliowasajili kwa fedha nyingi hawana msaada na timu hiyo.
Chanzo cha makini kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumatatu kuwa, bado viongozi wa timu hiyo ambao wana uhakika wa kubaki madarakani mara baada ya uchaguzi, wanaendelea kuangalia ni vijana gani watakaowafaa zaidi klabuni hapo bila ya kutumia pesa nyingi.
0 comments:
Post a Comment