Talib amshawishi Malkia wa Nyuki Simba
MWANAMAMA aliyetingisha nchi akiwa na klabu ya Simba, Rahma Al
Kharoos ‘Malkia wa Nyuki’ amepigiwa chapuo kuwa anaweza kuiongoza klabu
hiyo kwa mafanikio.
Malkia wa Nyuki kiongozi na mjumbe wa Kamati
Utendaji ya Simba, ndiyo alikipeleka kikosi hicho nchini Oman kwa ajili
ya kambi ya wiki mbili.
Akizungumza na Mwanaspoti, Talib ambaye ni kocha
na mchezaji wa zamani wa Simba na mtu wa karibu wa Malkia wa Nyuki kwani
wote wanaishi pamoja nchini Oman.
Alisema: “Kwa namna ninavyomjua Rahma (Malkia wa
Nyuki) kama ataamua mwenyewe aiongoze Simba, timu itakuwa na mafanikio
makubwa kwa sababu ni mpambanaji na anajua kazi. Lakini sijui kama yeye
mwenyewe atakuwa tayari kwa namna ninavyojua, huwa ana majukumu mengi
kwenye biashara zake na mambo mengine, anaweza asiwe tayari,”alisema
Talib.
Hata hivyo, Mwanaspoti ilimtafuta Malkia wa Nyuki
ambaye huwa anazunguka nchi mbalimbali kwa sababu ya shughuli zake,
haikufanikiwa.
Talib ambaye ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya
Oman ya soka la Ufukweni, alikwenda mbali na kusisitiza, atamshawishi
Malkia wa Nyuki ili utakapofika wakati wa uchaguzi, achukue fomu ya
uongozi wowote.
0 comments:
Post a Comment